SIKU Chache kupita baada ya Profesa Ibrahimu Lipumba kutangaza kujiuzulu nafasi ya uwenyekiti ndani ya Chama cha wananchi CUF, Hatimaye Chama hicho kimeunda kamati ya mda itakayodumu kwa miezi sita ili kusimamia nafasi za uongozi .Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo
Hatua hiyo imetangazwa mda huu Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif ambaye ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakati wa mkutano na waandishi wa Habari mara baada ya kumalizika Kikao cha Dharura cha Baaraza la kuu la uongozi wa chama hicho kilichoitishwa kujadili hatua hiyo ya kujiuzulu Profesa Lipumba.
Ambapo Seif amesema katokana na Kanuni za CUF wamefikia kwa pamoja kuunda kamati maalum itakayosimamia chama kwa kipindi cha Miezi sita na baadae kufanya uchaguzi wa nafasi hiyo ya uenyekiti.
Amesema Kamati hiyo itakuwa chini ya Katibu wa CUF ambaye ni yeye Maalim Seif na mwenyekiti wake atakuwa Mbunge wa Afrika Mashariki Twaha Taslima na Kamati hiyo itakuwa na kazi ya kukijenga chama hicho,pamoja na kushirikiana na Vyama vyengine vinavyounda UKAWA ambapo anadai itakuwa na jukumu lingine la kuhakikisha wanaitoa CCM madarakani.
No comments:
Post a Comment