Hamad Rashid Pamoja na Chifu Yemba mara baada ya kuchaguliwa kugombea nafasi za juu ya nchi katika uchaguzi mkuuu ujao |
Wakati vyama mbalimbali
viukiendelea kujiweka sawa kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka
huu nacho chama kipya katika uchaguzi huu chama cha ,,,,,,,,,ADC leo
kmimetangaza wagombea wake wan a fasi ya urais wa Zanzibar pamoja na mgombea wa
urais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Baada ya mchakato mrefu
wa kupitia na kusikiliza hoja za watia nia mbalimbali katika nafasi hiyo
mchakato uliopitia katika vikao vyote vya chama hicho hatimaye mkutano mkuu uliofanyika leo
umepitisha jina la chief liemba kuwania nafasi ya urais wa jamhuri ya muun gano
wa Tanzania huku jina la mlezi wa chama hicho HAMAD RASHID likipita bila
kupingwa kuwania nafasi ya urais wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar kupitia
chama cha ADC.
Maadhimio hayo
yamefikiwa leo jijini Dar es salaam katika mkutano mkuu wa chama hicho ambapo
wanachama walipiga kura ya kuwa na imani na wagombea hao kuipeperusha bendera
ya chama hicho katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mnamo tarehe 25 ya
mwezi wa kumi mwaka huu.
Akizngumza na wanachama
mara baada ya kuchaguliwa kunai nafasi hgiyo kubwa ya uongozi katika jamhuri ya
muungano wa Tanzania chief liemba amesema kuwa ana imani kubwa sana kuwa
atafanikiwa kushinda nafasi hiyo huku akitamba kuwa hadi sasa hajaona mgombea
kutoka chama chochote nchini ambaye ana uwezo wa kupambana naye katika uchaguzi
huo.
Kiongozi huyo ambaye
aliwahi kuwa mwenyekiti wa chama cha wananchi CUF mkoa wa shinyanga kabla ya
kutimkia ADC amesema kuwa ana uzoefu mzuri sana na siasa za Tanzania hivyo
hakuna mwanasiasa anayeweza kumsumbua kwa hoja huku akiwaahidi ushindi
wanachama na wapenzi wa chama hicho.
Mwenyekiti wa chama cha ADC ambaye sasa ni mgombea mwenza wa urais akizngumza na wanachama wa chama hicho wakati wa mkutano mkuu leo |
Naye mgombea wa Urais
katika serikali ya mapinduzi ya Zanzibar ambaye hapo awali alikuwa ndani ya
chama cha wananchi CUF mh HAMAD RASHID amesema kuwa sasa Zanzibar hakuna upinzani
kwani chama Tawala CCM pamoja na CUF wameungana na kuunda serikali hivyo chama
cha ADC kimekuja kutoa upinzani wa kweli na bhatimaye mwaka huu kufanikiwa
kuchukua dola hiyo.
Aidha katika hatua
nyingine mgombea urais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia chama hicho
chief liembe amemteua mwenyekiti wa chama hicho bwana SAID MIRAJ kuwa mgombea
mwenza wa urais katika uchaguzi ujao
No comments:
Post a Comment