Wateja wa kampuni
ya Tigo sasa wanaweza kutuma na kupokea fedha kupitia simu zao za mkononi kirahisi
na kwa haraka kutokana na maboresho makubwa ambayo kampuni hiyo imefaniyia
huduma yake ya Tigo Pesa.
Hii ni kwa mujibu wa taarifa
iliyotolewa leo na Tigo jijini Dar es Salaam kwa vyombo vya habari ikisema
kwamba maboresho hayo pia yamerahisiha ulipiaji wa ankara za huduma mbalimbali
ikilinganishwa na ilivyokuwa kabla.
“Tunayofuraha kuwatangazia
wateja wetu kwamba baada ya zoezi la maboresho kukamilika kwa ufanisi sasa
huduma za Tigo Pesa zimerejea,” ilisema
taarifa hiyo. Huduma za Tigo Pesa zilisitishwa usiku Jumamosi, Septemba 12 hadi
Jumapili mchana, Septemba 13 ili kufanya majaribio ya maboresho ya mtandao.
Tigo Pesa ni huduma maarufu ya kifedha
ikiwa na wateja zaidi ya milioni nne nchini kote.
Huduma zinazotolewa na Tigo
Pesa ni kutuma na kupokea fedha miongoni mwa wateja wa Tigo na kwa wateja wa
mitandao mingine ya simu, kuhamisha fedha kutoka kwenye akaunti ya simu kwenda
benki na kutoka kwenye akaunti ya benki kwenda simu ya mkononi, kulipia huduma
mbalimbali.
Mwaka jana Tigo ilikuwa kampuni ya kwanza duniani
kuanzisha huduma ya kutuma na kupokea ya kimatifa kwenda nchini Rwanda baina ya
watumiaji wa Tigo Pesa nchini na Tigo Cash nchini Rwanda. Tigo pia ilikuwa ya
kwanza mwaka 2014 duniani kuanza kulipa faida kwa watumiaji wa Tigo Pesa kutokana
na kiasi cha amana kilichoko katika akaunti ya mteja. Malipo haya hufanyika kila
baada ya miezi mitatu
No comments:
Post a Comment