Na OPTATUCY STAN wa dar es salaamMgombea wa urais
anayeungwa mkono na vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi UKAWA BW
EDWRD NGOYAI LOWASA amewaahidi wakazi wa
jiji la DAR ES SALAM kuwa kama atapewa ridhaa na wananchi ya kuwa rais wa
jamuhuri ya muungano wa Tanzania ataunda wizara maalum ambayo itakuwa
inashighulikia changamoto za jiji la dare es salaam.
Akizungumza na mamia
kwa maelfu ya wakazi wa eneo la chanika lililopo katika jimbo la ukonga llowasa
amesema kuwa anatambua kero za jiji la dar es saalam ndomaana kama atapewa
idhini na wananchi atahakikisha anamteuwa waziri ambaye akillala akiamuka kazi
yake kubwa itakuwa ni kushughulika na kero ambazo zinawatesa wakazi wa jiji.
Lowasa ambaye aliwasiri
eneo la chanika majira ya 8:26 mchana katika viwanja vya magenge alilakiwa na
umati wa watu wengi tofauti na ilivyokuwa inadhaniwa awali.akizungumzia kuhusu
propaganda zinazotolewa na baadhi ya watu kuwa kam wananchi wakichagua upinzani
nchi itaingia kwenye machafuko LOWASA iliwaomba wakazi wa eneo hilo kupuuza
maneno hayo huku akisisitiza kuwa kama wananchi wataamua kumpa ridhaa
atahakikisha anaunda selikali ambayo itakuwa rafiki kwa watu wa kada zote.
Kwa upande wake
mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo
CHADEMA bw FREEMAN MBOWE aliwaomba wakazi wa eneo hilo kutoa ushirikiano
kwa wananchi wengine ambao tayari wameshaamua kufanaya mabadiliko ili waweze
kuwa sehemu ya wananchi wanaotaka kuingia kwenye selikali mpya inayojali haki
na misingi ya utawala bora.
Sanjali na hayo mbowe alimtaka mwenyekiti wa tume ya
taifa ya uchaguzi jaji DAMIAN LUBUVA kukemea kwa vitendo kauli iliyotolewa na
mjumbe wa kamati kuu ya chama cha mapinduzi bw Abdalla bulembo aliyoitoa mkoani
kigoma kuwa chama cha mapinduzi kitaachi nafasi zote ila sio urais,Mbowe
amesema kuwa tume ya taifa ya uchaguzi inapaswa kuzitolea maamuzi ya kiuhalisia
kauli kama hizo kwani mwisho wa siku zinaweza zikasababisha machafuko.
Mgombea
wa ubunge kupita ukawa jimbo la ukonga bw mwita waitara amesema jimbo la ukonga
analijua sana hivo wana ukonga hawapaswi kufanya makosa tena kama ambayo
wamekuwa wakiyafanya miaka mingine.waitara amesema kazi ni moja tu kwa wana
ukonga kuhakikisha mara baada ya uchaguzi anatangazwa kama muwakilishi wao
LOWASA IKIWA ZAKIEM.Lowasa
aliwasiri katika viwanja vya zakiem mbagar majira 11:30 huku akilakiwa tena kwa
maelfu na maelfu ya wakazi wa kitongoji chenye wakazi wengi cha mbagara jijini Dar es saalam,lowasa aliwambia wana mbagara
kuwa kama wakimchagua atahakikisha kila mwananchi anatengenezewa mazingira bora
ya kuwa na maisha bora huku akiahidi kuwa
elimu bora pamoja na kilimo cha kisasa vitawekwa mbele maana ndo sekta
zinazowahusu watanzania wengi.
MBATIA AKIWA ZAKIEM. Mwenyekiti
wa chama cha NCCR MAGEUZI BW JAMES MBATIA aliwambia wana mbagara kuwa ukawa
wakiingia madarakani watafanya kazi ambayo watumwa na wananchi tofauti na
wanachokifanya chama cha mapinduzi kwa sasa.Mbatia aliwasihi wakazi wa eneo
hilo kuwa kiti limoja kwa sasa ili waweze kuleta mabadiliko ya kweli.BW mbatia
ambaye pia ni mgombea wa ubunge kupitia umoja huo katika jimbo la vunjo
aliwataka watu wote kuungana bla kujali tofauti zao na kufanya mabadilo
yatakayowaletea neema ya maisha.
No comments:
Post a Comment