Rais na Mwanzilishi wa kampuni inayotengeneza kinywaji chenye virutubisho ya Trevo Bw.Mark Steven yupo nchini Tanzania kuangalia jinsi kinywaji chake kinavyoenea nchini huku akiwahimiza watanzania kutumia kinywaji cha Trevo chenye virutubisho takribani 174 katika mwili wa binadamu.
Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es salaam leo Mark amesema kwamba Kinywaji cha Trevo ni kinywaji kilichotengenezwa kwa ubora wa hali ya juu uliohusisha vyakula mbalimbali nyenye kiwango kikubwa kutoka mataifa mbalimbali duniani.
Bidhaa hiyo imethibitishwa na mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA pamoja na Shirika la Viwango nchini (TBS),Kinywaji hicho kinasambazwa nchini kwa njia biashara ya Mtandao ambapo hadi sasa ni zaidi ya wanachama elfu tatu wamejiunga nchini Tanzania.
Muonekano wa kinywaji hicho |
Mkurugenzi huyo anataraji kutembelea katika mikoa minne ya Dar es salaam,Mwanza,Arusha,Mbeya ambapo mikoaa hiyo kuna maduka ya kiinywaji hicho ambacho amekitaja kama kinywaji bora ambacho kina uwezo wa kutibu magonjwa mbalimbali katika mwili wa binadamu
Kufuatia mahitaji kuwa makubwa kampuni hiyo inatarajia kufungua tawi lingine mkoani Mbeya siku ya jumatatu Sept 7,2015 ambapo inasambazwa pia katika mikoa ya Dar es salaam, Arusha na mkoani Mwanza.
No comments:
Post a Comment