Shirika lisilo la kiserikali
la linalotoa msaada wa kisheria kwa wanawake nchini WLAC kwa kudhaminiwa na OXFARM leo wameendelea na utaratibu wa kutoa mafunzo
kwa makundi ya watu mbalimbali nchini kuhusu mchakato mzima wa uchaguzi mkuu na
jinsi gani makundi hayo yanaweza kuutumia uchaguzi huo kupata viongozi
wanaowataka.
Baada ya wiki iliyopita
shirika hilo kuwakutanisha wakina mama mbalimbali ambao walikuwa viongozi wa
VICOBA wilaya ya kinondoni hatimaye leo shirika hilo limewakutanisha wanafunzi
wa vyuo vikuu mbalimbali nchini ambao kwa pamoja wamepata na kubadilishana
mawazo jinsi ya kushiriki kikamilifu katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Mwezeshaji wa mafunzo hayo Bi FORTUNATA MAKAFU akiendelea kutoa mafunzo mbalimbali kwa wanafunzi wa vyuo waliojitokeza katika mafunzo hayo Leo Jijini Dar es salaam |
Akizungumza na wanahabari
wakati wa mafunzo hayo leo mmoja wa wawezeshaji wa mafunzo hayo Bi FORTUNATA
MAKAFU amesema kuwa pamoja na ushiriki wa vijana katika uchaguzi huu kuonekana
ni mkubwa lakini bado changamoto kubwa ipo kwa vijana hao kugombea nafasi
mbalimbali za uongozi ambapo amesema hilo bado ni changamoto kwani vijana wengi
wamehamasika katika uchaguzi lakini bado hawajahamasika kuwania nafasi kama za
udiwani na ubunge.
Washiriki wakisikiliza kwa Makini |
Amesema kuwa lengo la
mafunzo hayo ni kuendelea kuwajengea uwezo vijana hao na kuwapa hamasa ya
kushiriki kikamilifu katika mchakato wa uchaguzi wa mwaka huu ili waweze
kuwachaguzi viongozi ambao watawasaidia katika kuwakwamua na hali iliyopo sasa.
Aidha amesema kuwa moja
ya mambo ambayo wanajaribu kuwaelekeza vijana kwa sasa ni kuwa wachambuzi wa
mambo hasa kipindi hiki cha kampeni kwa kusikiliza na kuchambua ni kiongozi
yupi ana uwezo wa kuwasaidia kwa dhati na kuepuka muhemko ya kisiasa ambayo
inaweza kuwapatia vijana viongozi ambao hawana nia dhabiti kwa watanzania.
Mshiriki DYNA STEVEN ambaye naye amekiri kupata msaada mkubwa wa kimawazo na kifikra katika mafunzo hayo ya leo |
No comments:
Post a Comment