Sunday, September 6, 2015

ZOEZI LA KUWAPOKEA WAKIMBIZI KUTOKA BURUNDI LAENDELEA VIZURI KATIKA KAMBI YA WAKIMBIZI NYARUGUSU MKOANI KIGOMA

Wakimbizi kutoka nchini Burundi wakipanga mizigo yao katika kambi ya Nyarugusu wilayani Kasulu mkoani Kigoma ambapo wamehifadhi wa kwa muda kabla ya kuhamishiwa kwenye kambi za Nduta, Karago na Mtendeli ikiwa ni mkakati unaoratibiwa naWizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la kushughulikia Wakimbizi (UNHCR) na mashirika mengine ya kimataifa ili kuwapatia makazi salama.

Mtoto Jamine Nibetanga (14), kutoka nchini Burundi akiandaa chakula katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu B iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma ambapo wakimbizi kutoka nchini Burundi wanahifadhiwa kwa muda kabla ya kuhamishiwa kwenye kambi za Nduta, Karago na Mtendeli

Mkimbizi kutoka nchini Burundi, Kukimana Dafroza (katikati), akifuma kikapu kama alivyokutwa katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu B iliyopo wilayani Kasulu mkoani Kigoma ambapo wakimbizi kutoka Burundi wanahifadhiwa kwa muda kabla ya kuhamishiwa katika kambi nyingine. Wengine ni Mkabanura Eviline (kushoto) naNiragira Dafroza (kulia).

Watoto wa wakimbizi kutokanchini Burundi wakichota maji jana katika moja ya vituo vya maji vilivyo wek wa katika kambi ya wa kimbizi ya Nyarugusu B iliyoko wilayani Kasulu Mkoani Kigoma ambapo wanahifadhiwa kwa muda.  Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi inampango wa kuwahamishiwa katika kambi za Karago, Mtendeli na Nduta ilikupunguza msongamano uliopo katika Kambi ya Nyarugusu

Mkimbizi kutoka nchini Burundi, Jacqueline Elulu (mwenyemtoto), akisubiri kupata huduma ya afya katika kituo cha Red Cross kinachotoa huduma za afya kwa wakimbizi walioko katika kambi ya Nyarugusu iliyoko wilayani KasulumkoaniKigoma. Shirika la Red Cross ni moja wapo ya wadau wanaoshirikiana na Serikali kutoa huduma za afya katika kambi ya Nyarugusu.

Mkimbizi Joseph Mtagura aliyeko katika Kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu akiandaa mihogo ya kuwauzia wakimbizi wenzake wanaoishi katika kambi ya Nyarugusu iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma

Mkimbizi kutoka nchini Burundi, Ntirampeba Acquelina akianika mihogo ambayo huwauzia wenzake katika kambi ya Nyarugusu B iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma. Ugali wa mihogo ni moja wapo ya vyakula muhimu vinavyotumika katika kambi ya Nyarugusu

Watoto wa wakimbizi kutoka nchini Burundi wanaohifadhiwa katika kambi ya Nyarugusu wakicheza mpira kama walivyokutwa jana na mpiga pichawaWizaraya Mambo ya Ndani ya Nchi.  Wakimbizi hao wamekua wakiingia nchini kutokana namachafuko ya kisiasa yaliyotokea nchini Burundi hivi karibuni
Wakimbizi kutoka  Burundi walioko katika Kambi ya Nyarugusu wakiandaa mboga ya kisamvu kama walivyokutwa na mpiga picha wa Wizaraya Mambo ya Ndani ya Nchi aliyeko katika ziara katika kambi hiyo
Mkimbizi Haveri manaEjide (kushoto) na mkewe Kugima na Evonapamojanawatotowaowakipatachakula cha mchanakatikakambiyawakimbiziyaNyarugusu B iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma ambapo wanahifadhiwa kwa muda kabla ya kuhamishiwa maeneo mengine ilikupunguza msongamano uliopo katika kambi ya Nyarugusu
Mkuu wa kambi yaWakimbizi ya Nyarugusu B iliyopo wilayani KasuluMkoaniKigoma, Fredrick Nisajile akiongea na wakimbizi walio katika mpango wa kuhamishiwa kwenye kambi za Nduta, Mtendeli na Karago.Wakimbizi hao waliopokelewa kutoka nchini Burundi hivi karibuni kwa sasa wanahifadhiwa kwa muda katika kambi ya Nyarugusu

No comments: