Friday, October 23, 2015

VIDEO--BAREGU ATOA NENO MASAA MACHACHE KABLA YA UCHAGUZI,TIZAMA HAPA


Umoja wa katiba ya wananchi UKAWA kwa kupitia chama cha Democrasia na maendeleo CHADEMA wamewashukuru watanzania kwa kuwaunga mkono katika kampeni zao za wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi ikiwemo za Urais,Ubunge na Udiwani kote nchi nzima na kusema kuwa wamefanya kampeni za kistarabu na zisizo na matusi wala fujo kama walivyoahidi wakati wanaanza.



Akiangumza na wanahabari mapema leo mjumbe wa kamati kuu wa CHADEMA Profesa Mwesiga Baregu amesema kuwa mgombea wao wa urais ambaye ni Mh EDWARD LOWASA amefanya kamoeni za kistarabu na za hadhi yake pamoja na matusi na kashfa za kizushi alizokuwa anashushiwa na wapinzani wake huku akiwashukuru watanzania kwa kuwaunga mkono kwa kipindi chote cha kampeni.



Aidha BAREGU amezngumzia hali halisi ya kisiasa kwa sasa nchini kuelekea uchaguzi mkuu unaotaraji kufanyika jumapili nchini kote hku akisema kuwa imani yake ni kuwa chama hicho kinakwenda kushinda uchaguzi huo bila wasiwasi na kuwaomba watanzania kujitokeza kwa wingi katika vituo vya kupiga kura ili waweze kufanya mabadiliko wanayoyataka.CHINI KUNA VIDEO NZIMA UNAWEZA KUITAZAMA

No comments: