
Unaweza ukadhani kuwa
watanzania wanaishi kwa furaha na upendo mkubwa kwa kuwatizama nyuso zao,lakini
laiti kama kungekuwa na uwezo wa kupima mtanzania mmoja mmoja kutizama mioyo
yao inawaza nini na kufikiria nini hakika tungeogopana hata kusalimiana kwa
kuogopa kuwa lolote linaweza kutokea.
Siasa za Tanzania ni
siasa ambazo tumeaminishwa kuwa ni siasa za kistaarabu na za kuheshimiana huku
tukiongozwa na wimbo maarufu sana ambao watu wameanza kuchoka kuuimba wa
TUITUNZE AMANI YETU,NA UMOJA WETU.Ni ukweli ulio waazi kuwa utambulisho mkubwa
wa mtanzania popote alipo ni amani na mioyo yetu ya ukarimu tuliyopewa kama
zawadi kutoka kwa mwenyezi mungu na tumekuwa tukiishi kwa misingi ya kuamini
kuwa bado mioyo hiyo tunayo huku tukiwa hatujui tunawaza nini ndani yetu.
Tuachane na hayo ambayo
nahisi hata nikiendelea kuyaeleza unaweza kukasirika na kuacha hata kusoma
nilichokusudia kuandika kwa siku ya leo,ni wiki takribani mbili na zaidi zimekatika
tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa Tanzania ambao ulifanikiwa kutupatia
watanzania Rais Mpya na wabunge pamoja na madiwani na nachukua nafasi hii
kuwapongeza wale wote ambao walichaguliwa na kupata nafasi ya kuiongoza Tanzania
bila kujali walioshindwa wanasemaje.
Tukiwa tunaongozwa na
kauli mbiu ya KUNA MAISHA BAADA YA UCHAGUZI kauli ambayo kwa kuisikiliza kwa
harakani kauli nikauli ambayo inatufanya watanzania tuendelee kujenga umoja
wetu na undugu ambao umekuwa ni kama nembo ya mtanzania,lakini ukijaribu
kuchambua maisha ya watanzania baada ya uchaguzi utagundua kuwa kauli mbiu hiyo
kila mtu anaweza kuitumia kutokana na mazingira husika.
Tukiwa katika maisha
baada ya uchaguzi siasa za Tanzania na vijana wa kitanzania wamepata pigo kubwa
sana ambalo halikustahili kutokea katika kipindi hiki ambacho tunaamini
uchaguzi wa Tanzania umemalizika kwa amani na tayari tumeanza kujenga umoja
wetu ambao ulitoweka wakati wa uchaguzi.
Kwa watanzania wapenda
siasa za harakati na watanzania wote hawawezi kushindwa kumfahamu ALPHONCE
MAWAZO ambaye mbali na kuwa kiongozi wa CHADEMA mkoa wa GEITA pia amewahi kuwa
kiongozi wa CCM na Diwani mkoani arusha hivyo imani yangu ni kwamba watanzania
wote wameguswa na kifo cha mwanaharakati huyu.
Kinachosikitisha kwa
sasa sio kifo cha Bwana MAWAZO ila kinachosikitisha wengi kwa sasa ni aina ya
kifo alichokufa,unaweza ukajiuliza hivi Tanzania hii imekosa amani kiasi kwamba
mtu unaweza kushambuliwa na watanzania wenzako mchana kweupe hadi wanakuondoa
uhai wako na wanatokomea kusikojulikana.
Unaweza kujiuliza hivi Tanzania
hii amani imetoweka kwa kiasi hiki hadi inafika mahali watanzania ambao
tunaishi nao mitaani wanaweza kukuweka katikati na mapanga wakakukatakata hadi
kukusababishia mauti na wakatoweka na baadae vyombo husika vikaja na taarifa
ile ile ya uchunguzi unafanyika kuwabaini wahusika wimbo ambao umeimbwa tangu
enzi za HAINES KIWIA NA WENJE,kuvamiwa mwanza,umeimbwa tangu enzi za DK ULIMBOKA
umeimbwa tangu enzi za ABSALUM KIBANDA, umeimbwa kwa mwanahabari MWANGOSI hao
wale na wengine ambao hata nikiwataja hapa ni kwazidishia watanzania
machungu,bado tunasubiri uchunguzi wa kubaini wahusika.
Hivi watanzania hawa
ambao tunawaaminisha kuwa wao ni watu wa amani na upendo waendelee kusubiri
uchunguzi ufanyike juu ya kifo cha ALPHONCE MAWAZO ambaye watu wameshughudia akiuwawa
na wananchi ambao kwa silaha za jadi,hivi watanzania hawa watakuwa na mioyo
migumu kasi gani ili waendelee kuamini kuwa Tanzania kuna amani ilihali watu
wamepoteza ndugu zao na wanaona kabisa hakuna haki iliyotendeka.
Nilipokua mdogo mtaani
kwetu aliwahi kushambuliwa kiongozi Fulani wa moja kati ya vyombo vyetu vya
usalama,nilichokishughudia kipindi hicho ni msaka mkoali ulioendeshwa mchana na
usiku na walifanikiwa kiwakamata wote waliohusika na walipelekwa mahakani siku
mbili baadae na sheria ilichukua mkondo wake,hivi hili la viongozi wetu wa
kisiasa ambao wana umati mkubwa unaaowaamini inashindikanaje kufanyika jambo
kama hili.
Watanzania wengi
ukizngumza nao kuna baadhi ya maneno wamechoka kuyasikia,mfano uchgunguzi
unaendelea,watu wasiojulikana,kesi ipo Mahakamani,ameachiwa kwa dhamana,hakimu
wa kesi anaumwa hivyo imesogezwa mbele,na maneno mengine ambayo yamekuwa
yakitokea baada ya matukio makubwa kama haya kutokea na mwisho wa siku picha
inamalizika kama filamu isiyokuwa na muongozaji.
Nasema haya kama
tahadhari nikiwa nina imani kubwa sana na serikali mpya kuwa inaweza ikaja na
majibu ya matatizo haya ambayo kama yakiachiwa yaendelee kutokea na tukaendelea
kuwapumbaza watanzanian na wimbo wa AMANI YETU historia itatuhukumu,hili la
GEITA sio tukio la kwanza kuondoka na roho ya mtu bila sababu yoyote na vyombo
husika vikanyamaza.
Jeshi la polisi hili ni
jaribio la kwanza pamoja na serikali ya Rais wetu mpya Docta JOHN MAGUFULI,hapa
ndipo tunapotaka kuona serikali ikitenda haki na sio tu kutenda haki lakini
haki yenyee ionekane ikitendeka,tunaimani sana na serikali yetu mpya na
tunaimani na utendaji kazi wa kiongozi wetu wa nchi,nimeamua kumuomba ombi
maalumu awarudishe watanzania katika umoja wao kwa kuhakikisha kuwa hili la
Kuuawa kwa mwenyekiti wa CHADEMA huko GEITA rafiki wa watanzania ALPHONCE
MAWAZO linakuwa ni mfano na wahusika wote wanatiwa mikononi mwa polisi na haki
ionekane ikitendeka.
ASANTENI.
R.I.P ALPHONCE MAWAZO
No comments:
Post a Comment