Friday, November 6, 2015

KUZIONA TWIGA, MALAWI 1,000/= TU


Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limetangaza kiingilio cha shilingi Elfu moja (1,000)  ndio kitakachotumika kuingia kushuhudia mchezo wa kirafiki wa Kimataifa kati ya Timu ya Taifa Wanawake ‘Twiga Stars’ dhidi ya timu ya Taifa ya Wanawake Malawi utakaochezwa kesho Jumamosi, Novemba 7 katika uwanja wa Azam Chamazi.
Twiga Stars inayonelewa na kocha mzawa Rogasian Kaijage iliingia kambini wiki iliyopita ambapo imekua ikifaya mazoezi kila siku katika uwanja wa Karume kujiandaa na mchezo huo wa kirafiki wa kimataifa.
Katika mchezo huo, Twiga Stars itautumia nafasi hiyo kumuaga mshambuliaji wake wa siku nyingi Estha Chaburuma ambaye ni miongoni mwa waanzilishi wa Twiga Stars na sasa anastaafu rasmi kucheza mpira wa miguu.
Upande wa timu ya Taifa ya Malawi tayari imewasili jana jioni jijini Dar e salaam ikiwa na kikosi cha wachezaji 20 pamoja na viongozi nane ambapo leo jioni kikosi chake kitafanya mazoezi katika uwanja wa Karume saa 10 jioni.

No comments: