Tuesday, November 3, 2015

MBILI MPYA ZA KIMICHEZO KUTOKA TFF LEO HII


Kufuatia tishio la Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika (CAF) la kutaka kuifungia Zanzibar ushiriki wa shughuli za mpira duniani, Rais wa TFF Jamal Malinzi alihitisha kikao cha usuluhishi. Kikao hiki kilikuwa na washiriki toka pande zote za mgogoro ambao ulipelekea mambo ya mpira kupelekwa Mahakamani.
Kikao hiki kimefanyika leo katika Hoteli ya Courtyard Dar Es Salaam chini ya Uenyekiti wa Rais wa TFF,  Jamal Malinzi.
Baada ya kutambua uzito wa suala lenyewe ambalo lingeweza kupelekea Zanzibar kukosa ushiriki michuano ya CAF na CECAFA ili kunusuru soka la Zanzibar na Tanzania kwa ujumla, kikao kimefikia maamuzi yafuatayo:
1. Uitishwe mkutano mkuu wa Zanzibar Football Association (ZFA) wa dharura kujadili
1.1 Mwenendo wa kamati ya utendaji.
1.2. Mapato na matumizi ya ZFA.
1.3. Kuteua kamati ndogo ya kuandika upya Katiba ya ZFA.
2. Rais wa ZFA, Ravia Idarus, kwa mujibu wa Katiba ya ZFA, ndiye atakeyeitisha mkutano huo.
3. Kamati ya sasa inayoendesha ligi Zanzibar, itaongezewa wajumbe watatu watakoteuliwa na Rais wa ZFA.
Ili maamuzi haya yaweze kuwa na nguvu za kisheria na kikatiba, kikao kimeazimia kuwa mashauri yote yaondolewe Mahakamani sasa na waliohusika kufungua mashtaka hayo wamekubali kuyaondoa mara moja.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linazishukuru pande zote na wadau wote wa Mpira wa Zanzibar waliowezesha kufikia hatua hii muhimu katika maendeleo ya Mpira wa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.

Mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Wanawake ya Tanzania ‘Twiga Stars’ Estha Chaburuma ‘Lunyamila’ ataagwa rasmi katika mchezo wa kirafiki kati ya timu ya Taifa ya Tanzania ya Wanawake ‘Twiga Stars’ dhidi ya timu ya taifa ya wanawake ya Malawi utakaochezwa siku ya jumamosi katika uwanja wa Azam Complex Chamazi jijini Dar es salaam.
Chaburuma amekua ni miongoni mwa wachezaji waanzilishi wa Twiga Stars ambapo amekua akiitumikia timu hiyo tangu kuanzishwa kwake mpaka sasa timu inapojiandaa na mchezo dhidi ya Malawi.
Mwenyekiti wa Kamati ya Soka la Wanawake ya TFF, Amina Karuma amesema wameamua kutumia mchezo huo wa kirafiki kwa ajili ya kumuaga Chabruma ambaye amekua ni chachu ya maendeleo ya mpira wa miguu kwa wanawake, kutokana na kuwafanya wanawake wengi kujitokeza kucheza mchezo huo.
Naye kocha wa timu hiyo, Rogasian Kaijage amesema vijana wake wapo katika hali nzuri, wananadelea na maandalizi ya mchezo huo wa jumamosi, ambapo anaimani watautumia vizuri katika kumuaga mchezaji mwenzao wa siku nyingi.

No comments: