Kampuni ya Tigo Tanzania hivi karibuni
imetanga za kufikisha wafuasi milioni moja katika mtandao wao wa Facebook. Katika
ukarasa wake wa Facebook, www.facebook.com/TigoTanzania kampuni ilifikisha mfuasi wa milioni moja Jumapili Desemba 27 mwaka huu hapa
Tanzania.
Kutokana na ongezeko la matumizi ya mtandao
wa kijamii wa Facebook hapan chini, Facebook imekuwa mstari wa mbele katika matumizi kutoka na uzinduzi wa
Facebook katika lugha ya Kiswahili uliofanyika mwaka wa 2014 kwa ushirikiano wa
Tigo Tanzania na Facebook, ambapo wateja wanaweza kutumia Facebook kwa lugha ya
Kiswahili na Kiingereza kupitia simu zao za mkononi bila malipo yoyote ya ziada.
Ukurasa wa Facebook wa Tigo uliundwa
Juni 2011 na umekuwa jukwaa madhubuti wa kurambaza na wateja wake wapendwa ambapo
wanajifunza kuhusu huduma na bidhaa mpya za kampuni.
Hivi karibuni, Tigo Tanzania
imejishindia tuzo mbili katika Tuzo za Uongozi Bora (Tanzania Leadership Awards)
ambayo inatambua mashirika na watu binafsi katika uongozi. Tuzo hizo ni ya Ubora
wa bidhaa (The Hall of Fame in Brand Excellence), na Matumizi Bora ya Mitandao ya
Kijamii Katika Mauzo( Best use of Social Media in Marketing).
Tigo Tanzania inaongoza katika soko
la mawasiliano na imekuwa mstari wambele katika mitandao ya kijamii ambapo wateja
wamekuwa wakiuliza maswali na kujibiwa haraka. Hii imeufanya mtandao kuaminika sana
na wateja na kutumika kama mwendelezo wa huduma kwa wateja.
Kuhusu Facebook Mkurugenzi wa Tigo
Bwana Diego Gutierrez anasema. “Jukwaa letu la Facebook na Twitter (Tigo
TZ) limekuwa kitendea kazi muhimu ambacho kinatumika kujifunza kutoka kwa wateja wetu na jamii kwa jumla ambao wanakitumia.
Tunajivunia kwa kuweza kuyafikia mafanikio
haya, na tunawashukuru wateja wetu kwa kuwa naimani nasi.
Tigo, imedhamiria kubadilisha mtindo
wa maisha wakidijitali kwa kuwa letea wateja wetu ubunifu wa teknolojia maridha
wa. Hivi karibuni, tumezindua teknolojia ya 4G LTE hapa Tanzania ambayo ni intaneti
iliyona kasi kuliko zote pamoja na ofa ya aina ya simu yaTechno Y3 Smartphone inayotumia lugha ya Kiswahili.