Dr
Yash Gulati, Senior Spine and Joint Replacement Surgeon at Apollo Hospitals; Delhi
Na Mwandishi Wetu,
Maendeleo katika njia za ufanyaji kazi pamoja na
matumizi ya teknolojia yanavyokuwa kwa kasi yanaweza kutufanya tuamini
tumepunguza maumivu katika viungo vyetu vya mwili ila si hivyo. Tunatumia
magari, mitandao mbalimbali ambayo vizazi vilivyopita havijawahi kuota kutumia.
Mabadiliko haya mapya katika maisha yetu yenye msisitizo mdogo katika
uimarishaji wa viungo umechukua hatamu na kuathiri maisha yetu kwa maana mwili
wa binadamu ni ule ule toka miaka milioni iliyopita. Na hiyo inasababisha
kuongeza matukio mengi ya maumivu ya mgongo kwa sababu uti wa mgongo umekwisha
athirika.
Watu wengi lazima wakutwe na maumivu ya uti wa mgongo
walau mara moja katika vipindi vya maisha yao. Sehemu kubwa inayoathirika
katika uti wa mgongo ni sehemu ya chini kabisa na sehemu ya shingoni kwa sababu
sehemu hizo ndizo zina beba uzito mkubwa wa mwili kila siku. Sababu nyingine
zinazosababisha maumivu ya mgongo ni kuharibika kwa diski, mgandamizo katika
vertebra na kudhoofika kwa mifupa kutokana na upungufu wa tishu (osteoporosis)
kutokana na umri inaweza kusababisha mgandamizo wa vertebra na kusababisha ufa.
Zipo zaidi ya sababu 100 zinazoweza
kusababisha maumivu ya mgongo upande wa chini; matukio ambayo yanaweza
kusababisha maumivu mgongoni na yasitambulike. Sababu maalumu ya kuleta maumivu
ya mgongo inabaki kuwa ni kuharibika au kuvunjika kwa sehemu zinazounga uti wa
mgongo kutokana na pozi baya la ukaaji.
Watafiti wameonyesha kuwa ukaaji mbovu
katika viti au sehemu yoyote na kutofanya kazi inayoshughulisha misuli ya
mgongo kunachangia maumivu ya mgongo na hata udhaifu katika uti wa mgongo.
Maumivu katika mgongo na shingoni ni moja ya sababu za msingi za wafanyakazi
kuchukua likizo maofisini. Asilimia 50 ya wafanyakazi wanajikuta wakipata
maumivu ya mgongo na shingo mara moja kwa mwaka.
Kwa mujibu wa Dk. Yash Gulati, Mpasuaji Mwandamizi wa uti wa
mgongo na viungo kutoka hospitali za Apollo; Delhi, habari
njema ni kwamba asilimia 75 ya matatizo yote yanayohusisha maumivu ya mgongo
yanaepukika, na asilimia iliyobaki yana epukika, mengine yanatibika na mgonjwa
kurudi katika hali yake ya awali ndani ya muda mfupi.
Baadhi ya sababu za kwa nini kumekuwa na
ongezeko la matukio ya maumivu ya uti wa mgongo ni kutokana na mabadiliko ya
maisha kwa watu wanaoishi mijini. Wengi huwa wanaanza siku zao kwa kupoteza
muda mwingi kwenye magari.
Kuendesha gari kwa muda mrefu kunapelekea
maumivu katika sehemu ya chini ya mgongo. Kuepuka hilo, siti ya dereva
inatakiwa iwekwe vizuri. Kama kuna uwazi kati ya siti na mgongo wa dereva,
uwazi huo uondolewe aidha kwa kuweka mto au kusogeza kiegemeo cha kiti mbele.
Magoti yanatakiwa yawe juu kidogo. Hiyo inaweza kuwa hivyo iwapo utajaribu
kusogeza kiti mbele au nyuma. Kama upo uhitaji wa kuendesha gari muda mrefu
kama sehemu ya kazi, ni vyema kuendesha kupata mapumziko mafupi ya
kushuka na kujinyoosha na kisha kuendelea na safari. Wakati wa kushuka ni vyema
mguu uanze kufika chini na sio kuruka.
Sababu kubwa ya pili iliyogundulika katika
kuleta maumivu mgongoni ni hizi kazi za kukaa kwenye kiti muda mrefu
(white-collar job) ambazo wafanyakazi wanapoteza muda mwingi mbele ya kompyuta,
hawakai katika viti vile ipasavyo au wakati ofisi ina samani zinazoathiri
ukaaji wa wafanyakazi. Ni vyema kila mfanyakazi ahakikishe kiti chake kipo
katika kimo kinachoendana na meza yake ili kutoumiza mgongo. Kompyuta ziwe
katika umbali unaofaa ili kuepuka mtu kukunja mgongo ili aweze kusoma au
kuandika chochote katika kompyuta.
Uzito uliozidi kutokana na kutofanya
mazoezi kunaweza kupelekea maumivu ya mgongo pia. Kwa mujibu wa Dk. Yash Gulati, uzito uliozidi unapoleta
kitambi mara nyingi hupelekea kujikunja kwa mgongo na kuanza kuleta maumivu
katika viungo na maungio katika mgongo. Ni muhimu sana kwa kila mtu kuhakikisha
ana uzito sawia na urefu wake, ili kupunguza madhara ya kuathiri uti wa mgongo.
Sababu nyingine inayotokea mara kwa mara ya maumivu ya
mgongo ni kusogea au kuharibika kwa diski alisema Dk. Yash Gulati wa Hospitali za Apollo;Delhi. Hii
inatokea pale ganda la nje la diski lililo kama shokomzoba katikati ya mifupa
miwili ya vertebral,linapochanika na kusababisha uvujaji wa ute mwepesi
uliopo ndani. Kulingana na sehemu diski ilipo, inaweza kubana neva za uti wa
mgongo na kupelekea maumivu makali na kupooza kwa miguu na mikono. “asilimia
tisini ya wenye tatizo la diski kuharibika wanapewa huduma kwa njia maalumu ya
mazoezi ya viungo (physiotherapy) na mapumziko ya kutosha. Ni mmoja kati ya
kumi watakao hitaji upasuaji mdogo (discectomy) wa kuitoa ile diski iliyosogea
na kubana neva” alisema Dk. Gulati.
Apollo ni moja ya hospitali chache zilizofikia kiwango
cha juu cha ubora wa matibabu na kufurahia matunda ya katika eneo adimu la
upasuaji katika uti wa mgongo. Upasuaji wa kuondoa diski unafanyika kwa
kuchukua tahadhari kubwa ya kupunguza madhara ambayo mgonjwa anapona mapema
bila uvimbe mkubwa na pia kuweza kuendelea na kazi zake za kawaida.
Imetolewa na:
Dk. Yash Gulati, Mpasuaji Mwandamizi wa uti wa mgongo na viungo
kutoka hospitali za Apollo; Delhi.
No comments:
Post a Comment