|
Mwenyikiti mpya wa shirikisho la wanafunzi wa elimu ya juu nchini Tanzania TAHLISO Ndugu STANSLAUS PETER akila kiapo kulitumikia shirikisho hilo mbele ya mwanasheria HAMZA JABIRI leo Jijini Dar es salaam kuanza kazi rasmi ya kuwatumikia wanafunzi wa elimu ya juu nchini Tanzania |
Na Exaud Mtei (msaka
habari) wa Habari24 blog
Uongozi mpya wa
shirikisho la elimu ya vyuo vikuu nchini Tanzania TAHLISO umesema kuwa upo
tayari kumuunga mkono Rais wa Tanzania Dr John pombe magufuli kwa kasi
aliyoanza nayo na kuhakikisha kuwa elimu ya Tanzania hasa elimu ya vyuo vikuu
inakuwa ya ubora unaofaa na inaheshimika nchini Tanzania.
|
Makamu Mwenyekiti mpya wa TAHLISO Ndugu JUMA ALLY OMARI akila kiapo leo jijini Dar es salaam |
Akizungumza na
wanahabari mapema leo jijini Dar es salaam katika hafla fupi ya kuwasimika
viongozi wa shirikisho hilo wapya mwenyekiti mpya wa TAHLISO Tanzania Bw STANSLAUS
PETER amesema kuwa kwa miaka mingi elimu ya juu nchini Tanzania imekuwa haina
ubora unaotakiwa ikiwa ni pamoja na mitaala mibovu,ukosefu wa mokopo kwa
wanafunzi wengi jambo linalowakatisha tamaa wengi kusoma,ambapo amesema uongozi
wake umeona kasi nzuri ya serikali ya awamu ya tano na wapo tayari kushirikiana
na serikali kutatua changamoto za wanafunzi nchini.
|
Naibu katibu mkuu wa TAHLISO KHAMIS ELLY akiapa leo Jijini Dar es salaam |
Mwenyekiti huyo amesema
kuwa utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wa mwaka huu umeonyesha kuwa serikali ya
Magufuli inawajali wanafunzi kwani asilimia kubwa ya wanafunzi walipata mikopo
na wengine wanaendelea kupata mikopo huku akiwataka wanafunzi kutulia kwani
neema kwao inakuja kutokana na kasi ya uongozi huo mpya pamoja na ule wa
serikali ya awamu ya tano.
|
Katibu mkuu Mtendaji mpya wa Shirikisho hilo SAGOLE WAMBURA akiapa leo |
Viongozi wa TAHLISO
wameapishwa leo rasmi Jijini Dar es salaam baada ya uchaguzi wa Kidemocrasia
uliofanyika tarehe 23 mwezi huu na wataiongoza Taasisi hiyo kwa mwaka mmoja kwa
mujibu wa katiba yao.
|
JOSEPH SHABAN ambaye ni muazini mpya wa shirikisho hilo Akiapa leo |
|
Omary Idd Naibu muazini akiapa leo tayari kulitumikia shirikisho hilo |
|
Mwenyikiti mpya wa shirikisho la wanafunzi wa elimu ya juu nchini Tanzania TAHLISO Ndugu STANSLAUS PETER akizungumza na wanahabari mara baada ya kuapishwa rasmi kuwatumikia wanafunzi wa elimu ya juu nchini |
|
Wanahabari waliokuwa katika hafla hiyo |
|
Picha za pamoja baada ya kula kiapo kwa viongozi hao wapya wa TAHLISO leo Jijini Dar es salaam |
No comments:
Post a Comment