Tuesday, December 22, 2015

KADCO YAOKOA ZAIDI YA BILIONI 2 UWANJA WA NDEGE WA KIA NDANI YA WIKI MOJA

Kaimu Mkurugenzi wa KADCO ,Bakari Murusuri |(Katikati) kushoto kwake ni mkurugenzi wa shughuli mama za kiwanja na huduma KADCO,Christopher  Mukoma na kulia kwake ni Meneja usalama wa Kiwanja, Justine Kisusi walipokutana na wanahabari .
Kaimu mkurug4e3nzi wa KADCO ,Bakari Murusuri akizung4umza na wanahabari (hawako pichani ) kuhusu matukio mbalimbali yaliyojitokeza katika uwanja huo.
Uwanja wa ndege wa kimataifa wa  Kilimanjaro (KIA)
Eneo la ndani la uwanja wa ndege wa KIA.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.,

KAMPUNI ya maendeleo ya viwanja vya ndege (KADCO) inayosimamia uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) imekoa zaidi ya kiasi cha sh Bil 2 katika kipindi cha wiki moja ikiwa ni thamani ya nyara za serikali na vito vya thamani vilivyokuwa vitoroshwe kupitia uwanja huo.

Menejimenti ya uwanja huo kupitia kitengo cha usalama kiwanjani hapo ilifanikiwa kukamata  kunasa vipande 264 vya madini ya Tanzanite vikiwa na uzito wa kilograamu 2.04 ambavyo thamani yake inakadiriwa kufikia Bilioni 2.5.

Vingine vilivyokamatwa uwanjani hapo vikiwa njiani kusafirishwa kuelekeaa nchini Vietnam ni pamoja na kucha 261 ,meno 60 ya Simba ambayo yanadaiwa kutokana na kuuawa kwa Simba 13 .

Kaimu mkurugenzi wa KADCO,Bakari Murusuri aliiambia Globu ya jamii kuwa Desemba 18 ,maofisa usalama uwanjani hapo walimkamata abiria mwenye asili ya Uarabuni akiwa na pembe mbili za Twiga.

“Siku ya Ijumaa tulimkamata abiria mwingine mwenye asili ya kiarabu,akitaka kutorosha pembe mbili za Twiga na baada ya tukio hilo Jumamosi katika ndege ya Ethiopian airlines walikamatwa abiria wengine raia wa kigeni wakitaka kutorosha Pembe mbili za Impala nao walishikiliwa na kukabidhiwa kituo cha polisi cha KIA.”alisema Murusuri.

Aliyekamatwa akiwa na Pembe za Tiwiga ametajwa na idara ya uhamiaji kuwa ni Jasim Mbarakke Alh-kubaisi (43) ambaye anaidaiwa kuwa ni mlinzi wa mfalme wa nchi ya Qatar iliyopo katika falme za kiarabu.

“Ukiangalia haya matukio ndani ya wiki moja ,tumeweza kuokoa kiasicha fedha zisizopungua Bilioni mbili za kitanzania,kama viongozi wengine katika viwanja vingine ,mipakani a taasisi nyingine ila mmoja atashuhudia serikkali yetu inavyoweza kujiondesha kwa kodi za ndani”aliongeza Murusuri.

Alisema katika uwanja huo kumekuwa na matukio mengi ambayo hayakuripotiwa kwenye vyombo vya habari yakiwemo ya kukamatwa kwa watu 11 wakisafirisha dawa za kulevya katika kipndi cha miaka miwli iliyopita.

“Matukio yamekuwa yakitokea mengi ,ndani ya miaka miwili iliyopita katika uwanja huu tumekamata watu wasio pungua 11 wakijaribu kupitisha dawa za kulevya na tayari wamefikishwa mbele ya vyombo vya sheria ikiwemo wengine kufungwa jela.”alisema Mrusuri.

Murusuri alisema kwa sasa katika uwanja huo kumefungwa vifaa vya kisasa ambavyo vinahakikisha kwa hakuna mtu anaye pita uwanjani hapo na vitu ambavyo havijaruhusiwa kisheria ikiwa ni jitihada za kumuunga mkono rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania ,John Magufuli.

Mapema wiki iliyopita jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro lilitoa taarifa ya kushkiliwa kwa watu wanne wakiwamo  raia wanne kutoka mataifa tofauti kwa makosa mbalimbali, akiwemo aliyekutwa na
nyara za serikali kinyume cha sheria.

Kamanda wa polisi mkoani hapa, Fulgence Ngonyani alisema tukio la kwanza lilitokea Dec 15 majira ya saa 10.00 alasiri katika uwanja wa
 ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), ambapo alikamatwa raia wa Vietnam,Hoang Nghia Trung(49) akitaka kusafirisha nyara hizo.

Alisema mtuhumiwa huyo alihifadhi nyara hizo katika mabegi yake ambapo maofisa wa usalama katika uwanja wa ndege wa KIA walimtilia shaka na kufanya upekuzi katika mabegi yake ndipo walipokuta nyara hizo zikiwa zimehifadhiwa ndani ya mabegi hayo.

Hata hivyo thamani halisi ya  nyara hizo bado haijajulikana na mtuhumiwa anaendelea kuhojiwa na atafikisha mahakamani mara upeleleziutakapokamilika.

Katika tukio jingine ,Anurag Jain(45) raia wa India alikamatwa uwanja wa ndege wa Kia akiwa na madini ghafi aina ya Tanzanite vipande 264 bila kibali akiwa amehifadhi kwenye mabegi yake akielelekea Hong Kong China.

Mwisho

No comments: