Meneja Ustawi wa Jamii na Mahusiano wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa ,Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) Jumaa Almasi akizungumza kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Dk, Othman Kiloloma wakati wa Maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kichwa Kikubwa na Mgongo wazi Duniani 2015. Maadhimisho hayo yamefanyika Moi katika hospitali ya Muhimbili jijini Dar es salaam na kaulimbiu ya mwaka hu inasema “PAMOJA TUZUIE ULEMAVU WA KUZALIWA” (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA) WA UJIJIRAHAA BLOG
Mwenyekiti na Mjumbe wa Kamati ya kusaidia watoto wenye ulemavu wa vichwa vikubwa na mgongo wazi wakishirikiana na Wafanya Biashara wa Soko la Kariakoo Mtaa wa Raha Sweya na Mhonda Jijini Dar es Salaam, Ludovick Mmasi akizungumza kwa niaba ya wenzake katika Maadhimisho hayo baada ya kuguswa na watoto wenye ugonjwa huo.
Mtoto Selemani Joseph (14) kushoto ambae ni mwanafunzi wa Darasa la Tatu katika Shule ya Mother Telesia iliyopo Kisiwani, Kigamboni Dar es Salaam akipozi na mwenzake katika ofisi za Chama hicho.
Wakifanya matembezi ya kuadhimisha maadhimisho hayo yaliyofanyika jijini dar es salaam.
No comments:
Post a Comment