Uchaguzi wa nafasi ya umeya katika jiji la Tanga umevurugika baada ya madiwani kwa kushirikiana na viongozi wa chama cha wananchi CUF kupinga matokeo yaliyotangazwa na msimamizi wa uchaguzi jimbo la Tanga wakidai kuwa yamechakachuliwa hatua ambayo imesababisha askari kukabiliana na vurugu hizo baada ya msimamizi kukimbia na kwenda kujifungia ofisini kwake kwa ili kunusuru maisha yake.
Wakizungumza kwa jazba katika uchaguzi huo baadhi ya wafuasi na viongozi wa chama cha wananchi CUF wamesema hawakubaliani na matokeo hayo kwa sababu wapiga kura wa CUF walikuwa 20 na wale wa ccm ni 17 lakini katika matokeo hayo msimamizi alitangaza kuwa mgombeanafasi ya umeya Selemani Mustapher wa CCM amepata kura 19 na Hamad Rashid Jumbe amepata kura 18.
Wakielezea kwa masikitiko kuhusu mchakato wa uchaguzi huo huku baadhi yao wakimwaga machozi baadhi ya wakereketwa wa CUF walioshiriki kuwaapisha madiwani siku moja kabla ya uchaguzi ili wasiweze kurubuniwa wamesema uchaguzi kama huo unaweza kusababisha maafa kwa sababu haukuwa wa haki na kweli.
Hata hivyo mgombea nafasi ya umeya kwa tiketi ya CCM Selemani Mustapher akizungumza katika zoezi hilo amewataka wananchi kuwa watulivu na ameomba ushirikiano baada ya kutangazwa na msimamizi wa wa uchaguzi jimbo la tanga Bwana Daud Mayeji.
No comments:
Post a Comment