TAARIFA CHAMA CHA
ACT-WAZALENDO KWA VYOMBO VYA HABARI
JUU YA MAUAJI
YANAYOENDELEA NCHINI BURUNDI
CHAMA
cha ACT-Wazalendo kinasikitishwa sana na maujai yanayoendelea nchini Burundi na
hasa Mji Mkuu wa nchi hiyo Bujumbura. Hali hii ya mauaji imesababishwa kwa kiasi
kikubwa na uamuzi wa Rais wa sasa wa nchi hiyo Ndugu Piere Nkurunzinza kuendelea
kugombea na hatimaye kuchaguliwa kuwa Rais wanchi hiyo katika mazingira yanayodaiwa
kuvunja demokrasia na utawala bora.
Tangu machafuko hayo ya
nchini Burundi yaanze zaidi ya watu 100 wameshauawa kufikia wiki hii na wengine
kadhaa kujeruhiwa.
Aidha, wimbi la
wakimbizi kutoka Burundi linarudi kwa kasi na wengi wao wakikimbilia nchini
Tanzania.
Bahati mbaya sana mpaka
sasa Jumuiya ya Kimataifa na hasa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo Burundi ni
mwanachama, haikuchukua hatua za maana za kuzuia kuchafuka kwa utawala wa kidemokrasia
na utawala washeria nchini Burundi, na wala haichukui hatua stahiki kuzuia mauaji
yanayoendelea.
Hii ni kinyume kabisa na
Mkataba unaounda Jumuiya ya Afrika Mashariki ambao unatoa kipaumbele cha juu kulinda
uhai na haki zaraia katika Jumuiya hizo
Kutokana na hali ya kisiasa
na usalama nchini Burundi, na kwa kuzingatia nafasi ya kihistoria ya Tanzania
katika kutafuta na kufanikisha Mkataba wa Amani nchini Burundi, na kwa kuzingatia
na fasi yake katikaJ umuiya ya Afrika Mashariki na Umoja wa Afrika, sis
ACT-Wazalendo tunaitaka serikali ya Tanzania, kwa hali kubwa ya dharura,
ichukue hatua zifuatazo:
1.Iitake serikali ya Jamhuri
ya Burundi kukomesha mara moja mauaji yanayoendelea nchini humo na kuwahakikishia
raia wanchi hiyo usalama
2.Tanzania Iitake serikali
ya Jamhuriya Burundi kuitisha mkutano wa wadau
wote wasiasa na utawala nchini humo ilikujadili mustakabali wa nchi hiyo
kisiasa na kijamii, ikiwemo uwezekano wa kuunda serikali ya Umoja wa Kitaifa itakayosimamia
Katiba ya Burundi kuelekea uchaguzi wa kidemokrasia
3.Tanzania Itumie nafasi
yake katika Jumuiya ya Afrika Mashariki kuitaka Jumuiya hiyo kuzuia machafuko nchini
Burundi na kuhakikisha kwamba utawala wademokrasia na utawala wa sheria unazingatiwa
nchini humo
4.Chama cha
ACT-Wazalendo kinasisitiza kuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki itakosa uhali wa kuendelea
kuwepo kwake kama itaendelea kuwa Jumuiya ya viongozi wa nchi zinazounda Jumuiya
hiyo huku ikishindwa kusimamia haki za kuishi na haki za kiraia za wananchi wa Afrika
Mashariki.
Imetolewa leo jumatano
16 Disemba 2015
Na VenanceMsebo
Katibu wa Kamati ya
Mambo yaNje
ACT-Wazalendo
No comments:
Post a Comment