Mmiliki wa moja ya GODAUNI la vifaa vya ujenzi KIWALANI
Jijini Dar es salaam katika mtaa wa KIGIRIGIRI GODAUNI NUMBER 117, BW. FURAHA
SALUM MAWAMBA ameilalamikia TANROAD kubomoa moja ya GODAUNI lake la vifaa vya
ujenzi bila kufuata sheria hivyo kumsababishia hasara ya BILLION MOJA.
Akizungumza na waandishi wa habari hii leo jijini
DAR-ES-SALAAM,MAWAMBA amesema anasikitishwa sana na kitendo hicho
walichokifanya Tanroad kwa madai ya mmiliki huyo kujenga godauni hilo mpaka
eneo la barabara,ambapo mmiliki huyo amekanusha kuwa sababu hizo sio za kwel,bali
wamefanya hivyo kwa makusudi baada ya kukataa kuwapa rushwa
“maofisa hawa wa TANROAD wamekuwa wakinifwatilia mara kwa
mara nakuhitaji rushwa lakini sikutishika na sikuwa tayari kwani navyojua eneo
langu lipo mbali na barabara hivyo leo wamebomoa sehemu ya Godown langu na
baadhi ya vifaa vyta ujenzi”.amesema mmiliki huyo.
Pia amesema kuwa maofisa hao wa TANROAD hawakupita katika
ngazi zinazohusika ikiwemo kwa vongozi wa serikali za mtaa huo kwa mjumbe wala
kwa diwani wa eneo hilo hivyo amemuomba Rais Magufuli kuweza kumsaidia kupata
haki yake kwani anaamini Rais ni msikivu na mtetezi wa wanyonge.
Mmiliki wa moja ya GODAUNI la vifaa vya ujenzi KIWALANI Jijini Dar es salaam katika mtaa wa KIGIRIGIRI GODAUNI NUMBER 117, BW. FURAHA SALUM MAWAMBA akiwaonyesha wanahabari baadhi ya nyaraka zinazompa uhalali wa kuwa katika eneo hilo lililobomolewa na TANROAD |
Akizungumza Diwani wa kata ya Kiwalani MUSA KAFANA amesema kuwa
kwa sasa anakusanya matatizo ya wananchi waliobomolewa kwa mmoja mmoja na ujumla
kuyapeleka kwenye vyombo vya sheria ili Kushughulikiwa kwa wakati huku diwani
huyo akikiri kutofwatwa na maofisa kwa ajili ya zoezi la ubomoaji na kusema zoezi
hili la ubomoaji ni Batili na uonevu kwa wananchi.
Aidha mmoja wa wananchi katika eneo hilo Mzee HERRY NDELELE
amesema kuwa serikali siku zote inapokuja kubomo huwa inatoa taarifa kwa
mmiliki wa jengo na uongozi wa mtaa hivyo anashangaa kuona zoezi hilo
likifanyika bila utaratibu huo huku akisisitiza serikali kumsaidia mmiliki wa
GODAUNI hilo na kumpa haki yake kwani sehemu aliyojenga ni halali na yupo nje
ya barabara
“Mimi ni mtu wa zamani sana katika mtaa huu nachojua barabara
hii imefuata wananchi na nashangaa kuona kitendo hiki cha kubomolea wananchi
kiholela na buila kutowapa stahiki zinazofanana na aamani ya mali zao”amessisitiza
STORY PICHA NA IZACK MAGESA-DAR ES SALAAM
No comments:
Post a Comment