Thursday, January 7, 2016

Hivi Ndivyo Mrithi wa Kamanda KOVA DCP SIMON SIRRO alivyoanza kazi




Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewataka wananchi hususani madereva, makondakta na abiria wanaosafiri kutoka kituo cha mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani kuwafichua waalifu wanaoingiza silaha ndogondogo, madawa ya kulevya, na wahamiaji haramu kupitia usafiri wa mabasi hayo.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Naibu Kamishna wa Polisi SIMON SIRRO ameyasema hayo leo alfajiri alipokuwa akizungumza na madereva, makondakta na abiria na kusema kuwa wahaalifu wengi wanatumia usafiri huo katika kutekeleza uhalifu wao bila kugundulika, na kuwataka wananchi kutoa taarifa zitakazo saidia kuwafichua waalifu hao.

Kuhusu suala la uingizaji wa silaha katika jiji la Dar es Salaam Kamanda SIRRO amesema silaha hizo zinaingizwa na wahaalifu kupitia usafiri wa mabasi toka nchi jirani zenye migogoro ya kisiasa na vita kama Burundi, Congo DRC na Somalia kupitia nchi ya Kenya ambapo zote kwa pamoja zinapakana na Tanzania.

Akizungumzia madawa ya kulevya alisema kuna changamoto kubwa ya kudhibiti biashara hiyo harama inayoleta madhara makubwa kwa jamii yetu. Amesema madawa ya kulevya mengi yanaingizwa nchini kupitia baharini na maziwa makuu kisha yanasafirishwa kwa usafiri wa mabasi kutoka mikoa ya pembezoni. Amewaomba wanachi kuwafichua wahalifu hao kwa kutoa taarifa polisi pindi wanapomtilia shaka mtu yeyote. 

Amewaasa watanzania kuacha utamaduni wa kuaminiana 
kupita kiasi na watu wasiowafahamu na kuwataka kutopokea vitu vidogo vidogo kama juice au maji ambvyo huchanganywa na madawa ya kulevya na kusababishwa kuibiwa au madhara mengine.

Aliwataka wananchi washirikiane na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa kupitia namba  0754 280 994 wakati wote ili kupata huduma stahiki.

SIMON SIRRO – DCP
KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM

DAR ES SALAAM

No comments: