Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye akiongea na wafanyakazi wa Wizara hiyo wakati wa kikao cha wafanyakazi kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye akimkabidhi cheti cha mfanyakazi mmoja wa wafanyakazi wa Wizara hiyo.
Waziri wa Habari ,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye kushoto akiongea na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo kulia Prof. Elisante Ole Gabriel kulia wakati wa mkutano wa wafanyakazi uliofanyika Dar es Salaam leo, katikati ni Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw. Leornard Thadeo.
Waziri wa Habari ,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Wizara hiyo mara baada ya mkutano na wafanyakazi hao.
(Picha na Benjamin Sawe-WHSUM)
…………………………………………………………………………………………..
Na Tiganya Vincent-MAELEZO-Dar es Salam
Waziri wa Habari, Utamaduni , Sanaa na Michezo Nape Nnauye amempongeza mchezaji wa mpira wa miguu wa Taifa Star Mbwana Samatta baada ya kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa soka Afrika 2016 kwa wachezaji wanaocheza soka Barani Afrika.iliyotolewa nchini Nigeria.
Nnauye ametoa kauli hiyo wakati wa mkutano na watumishi wa Wizara wa Habari, Utamaduni , Sanaa na Michezo leo jijini Dar es salaam.
Amesema tuzo hiyo imemjengea heshima na kuleta sifa kwa Mbwana Samatta mwenyewe, wanasoka hapa nchini na Tanzania kwa ujumla katika medali ya Soka Kimataifa.
Nnauye amewataka wachezaji wengine kufuata nyayo za mchezaji huyo kwa kuongeza juhudi, nidhamu katika michezo na watambue kuwa mchezo wa mpira wa miguu ni kazi kama zilivyo kazi nyingine.
Akifafanua zaidi Nnauye alibainisha kuwa kilichomfikisha Samatta hapo ni kujitambua na kujituma katika ajira yake.
Samatta ameibuka mshindi wa Tuzo ya Mchezaji bora wa mwaka kwa wachezaji wanaocheza ligi ya Barani Afrika kwa kupata alama 127 dhidi ya Robert Kidiaba aliyepata alama 88 na Baghdad Bounedjah alama 63.
No comments:
Post a Comment