Sheikh Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Sheikh Alhadi Mussa Salim akizungumza na wanahabari wakati wa Sherehe hizo zilizofanyika Jijini Dar es salaam. |
Na Exaud Mtei (Msaka
Habari)
Madhehebu ya kiislam Nchini
kote na duniani wametakiwa kujenga umoja wa kudumu,kukaa kwa pamoja na kujadIli
maswala yanayowahusu jambo ambalo litasaidia kuleta amani baina ya dini hiyo na
dunia kwa ujumla.
Rai hiyo imetolewa
Jijini Dar es salaam na sheikh Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Sheikh Alhadi Mussa Salim
wakati wa sherehe maalum zilizowakutanisha waislam wa Madhehebu ya shea na sun
kwa ajili ya kusherekea na kukumbaka kwa pamoja siku ya kuzaliwa kwa mtume muhammad
s.a.w Jijini Dar es salaam.
Akizumngumza katika
sherehe hizo Kiongozi huyo amesema kuwa kitendo cha madhehebu hayo mawili
kukutana na kukaa kwa pamoja ni ishara nzuri ya kuonyesha kuwa Dini sio uadui
bali ni umoja na uoendo hivyo akaitaka dunia kwa ujumla kutambua hilo.
Amesema kuwa hakuna
haja ya kuendelea kujenga chuki na uhasama baina ya madhehebu hayo bali jambo
sahihi ni kukaa kwa pamoja na kujadili
mambo yanayowahusu na yale yatakayoshindikana kutokana na itikadi za kidini
yaachwe ili yasiwe ni chanzo cha chuki mbalimbali.
Mmoja kati ya walimu wa Kidini ambaye alishiriki katika sherehe hizo MSABAHA SHABAN MAPINA akizngumza na wanahabari umuhimu wa kukutana kwa waislam wa imani tofauti |
Mtandao huu ulifanikiwa
kuzungumza na baadhi ya washiriki katika sherehe hizo ambapo mmoja wa walimu wa
kidini MSABAHA SHABAN MAPINA amesema kuwa sherehe ya kukutana kwa madhehebu
hayo mawili yenye imani Tofauti tofauti ni jambo la kuigwa na Tanzania nzima
pamoja na dunia kwani ni njia nzuri ya kujenga umoja wa kidini ambao ilikuwa
umeanza kutetereka
No comments:
Post a Comment