JANA limetokea tukio la aibu katika nchi yetu pale
serikali ilipofanya jaribio la hatari la kuzuia wananchi kuona na kusikia kinachoendelea
bungeni.
Kitendo cha serikali ya CCM kuzuia kuonyeshwa moja
kwa moja vipindi vya bunge katika televisheni ya taifa ni cha kijima na sisi
chama cha ACT-Wazalendo tunakilaani kwa nguvu zetu zote.
Tunakitafsiri kitendo hiki cha serikali kama mwendelezo
wa hatua na juhudi za Rais Magufuli za kuminya demokrasia na kusimika utawala
wa kiimla.
Tunawasihi wananchi kusimama imara na kuzipinga
jitihada zozote ovu za kuminya demokrasia nchini.
Tunawapongeza
wabunge wazalendo wa upinzani kwa kusimama pamoja na kupinga nia ovu ya
serikali ya kuua demokrasia katika nchi yetu.
Tunawatia shime
wabunge wote wazalendo kuendelea kupigania maslahi mapana ya taifa letu.
ACT-Wazalendo!
Taifa kwanza leo na kesho!
Samson
Mwigamba,
KATIBU MKUU.
No comments:
Post a Comment