Pichani ni washindi wa jumla wa tuzo za wanasayansi chipukizi za young Scientinsts wakikabidhiwa vyeti |
KATIKA kuinua sekta ya sayansi nchini,Taasisi ya Karimjee Jinavanje imewatunuku nafasi za masomo Edmound Luguku na John Method wanafunzi wa shule ya sekondari ya mzembe kuwa washindi wa jumla ya tuzo za wanasayansi chipukizi za Young Scientinsts Tanzania kwa mwaka 2015.
Hayo yametokea leo jijini Dar es Salaam wakati wa halfa fupi ya kuwaaga washindi hao,ambapo akiongea na wanahabari wakati wa halfa hiyo,Meneja wa taasisi hiyo,Devotha Rubuma amesema washindi hao wawili walipata fursa ya kupelekwa masomoni baada ya kumaliza kidato cha sita.
Ameeleza kuwa washindi watasafiri leo kuelekea Dubiln nchini Ireland ambapo watahudhuria maonesho ya kimataifa ya sayansi na Teknolojia ambapo kila mwaka hufanya mashindano yanayolenga kuhamasisha wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kupenda sayansi,
Kwa upande wake mwenyekiti wa heshima ya kundi la makampuni ya KarimjeeJivanje,Hatim Karijee amesema tuzo lengo la shindani hilo ni kutoa uwezo kwa watanzania,
“Tumepewa heshima kubwa sana kuweza kuwa sehemu ya tuzo za Young Scientist Tanzania kwani tunaamini kwamba elimu ni muhimu sana kwa mustakabali wa maendeleo ya Tanzania na pia kwa sababu elimu ya sayansi inaweza kuleta fursa nzuri kitaalum”amesmea Karimjee.
Karimjee ameongeza kuwa lengo la kimtazamo wa taasisi hiyo hivi sasa ni kuisadia taasisi za elimu kwa kuboresha uwezo wake,familia ya karimjee ilianisha taasis mbali mbali za misaada kwenye miaka ya 1950 kabla ya uhuru.
“Tumejenga shule nyingi ,hospitali ,zahanati na vituo vya huduma za kijamii ambazo mojawapo ya misaada wetu mkubwa ni ukumbi wa mkubwa wa Karimjee ambazo tuliujenga ambao tulilenga na kuutoa msaada kwa Halmashauri ya Manispaa ya Dar es salaam mwaka 1957”
No comments:
Post a Comment