Wednesday, February 3, 2016

LHRC WAMTAKA JECHA WA ZEC KUJIUZULU MARA MOJA,WAPINGA MARUDIO YA UCHAGUZI ZANZIBAR

Katikati ni kaimu mkurugenzi wa kituo cha sheria na Haki za binadamu Bi IMELDA LULU URIO akizungmza na wanahabari mapema leo kuhusu hali ya zanzibar,kushoto kwake ni wakili HAMIS MKINDI kutoka LHRC na kulia kwake ni Mwanasheria kutoka kituoni hapo  Anna Henga 
 Na Exaud Mtei (Msaka Habari)

Zikiwa zimesalia Takribani siku 18 kufanyika kwa marusio ya uchaguzi mkuu wa marudio visiwani Zanzibar,kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC wameibuka na kupina uchaguzi huo huku wakimtaka mwenyekiti wa tume ya uchaguzi wa Zanzibar JECHA SALUM JECHA kujiuzulu mara moja kwa kushinda kusimamia uchaguzi wa zanzibar na kusababisha kuvurugika kwa uchaguzi huo.

Katika mkutano na waandishi wa habari mapema leo kaimu mkurugenzi wa LHRC Bi IMELDA LULU URIO amesema kuwa hatua ya mwenyekiti JECHA kufuta uchaguzi bila kufuata sheria kunampunguzia sifa za kuongoza tume hiyo na ni kiashiria cha wananchi kukosa imani naye hivyo anatakiwa kuchukua hatua ya kujiondoa.

kaimu mkutugenzi wa kituo cha sheria na Haki za binadamu Bi IMELDA LULU URIO akizungumza na wanahabari mapema leo
Amesema kuwa kufutwa na kutangazwa upya kwa uchaguzi wa Zanzibar kunakiuka katiba,sheria,na kanuni za uchaguzi na pia misingi ya democrasia misingi ya utawala na sheria nchini.

Amesema kuwa katiba ya Zanzibar na sheria za uchaguzi hazijampa mamlaka mwenyekiti na hata tume yote kufuta uchaguzi na hivyo kilichotokea Zanzibar kimeaacha watanzania wakiwa hawaelewi ni sheria na katiba ipi imetumika kufanya swala hilo.

 Wakili HAMIS MKINDI kutoka LHRC 
“kwa mujibu wa kifungu cha 88 cha sheria ya uchaguzi zanizbar wasimamizi wa uchaguzi ndio wenye mamlaka ya kutangaza matokeo ya uchaguzi wa wajumbe wa baraza la wawakilishi na madiwani,jambo ambalo wasimamizi wa uchaguzi walishalifanya kwenye majimbo mengi ya uchaguzi kwa kuwatangaza washindi na kuwapatia vyeti kudhibitisha uhalali wao hivyo tunashangaa uchaguzi ulianza kuonekana sio halali wapi”amehoji wakili huyo msomi Kutoka LHRC

Bi IMELDA ameongeza kuwa kwa mujibu wa kifungu cha 123 cha sheria ya uchaguzi Zanzibar mtu akishachaguliwa uchaguzi wake hautohojiwa isipokuwa kwa kupeleka shauri mahakamani,hivyo kwa msingi huo LHRC wanaona kwamba hakuna kifungu chochote cha sheria kinachoipa tume ya uchaguzi au mwenyekiti wake mamlaka ya kufuta uchaguzi na kuamuru marudio isipokuwa kwa amri ya mahakama.

Aidha katika hatua nyngine LHRC wamehoji kuhusu mazungumzo yaliyokuwa yanaendelea yakiwahusisha wakuu wa nchi akiwemo Raisi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania DR JOHN POMBE MAGUFULI,Raisi wa Zanzibar DR ALLY MOHAMED SHEIN,Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Mh seif sharif Hamad,pamoja na marais wastaafu wa Tanzania ambapo wamesema kumekuwa na ukimya mkubwa baada ya yale mazungumzo ambapo watanzania hawakupewa taarifa halisi kuwa nini hasa kilikuwa kinazungumzwa katika mazungumzo hayo huku akisema wananchi wana haki ya kufahamu kila kitu kilichokuwa kinaendelea.

Wanahabari wakidaka Taarifa hiyo
Matokeo ya uchaguzi wa Zanzibar yalifutwa Rasmi na mwenyeiki wa tume ya uchaguzi wa Zanzibar JECHA SALUM JECHA kwa sababu kuwa kulikuwa na dosari kadhaa ambapo uchaguzi huo sasa utafanyika tarehe 20 mwezi wa pili huku chama cha wananchi CUF wakiwa tayari wameshajiondoa katika uchaguzi huo


No comments: