Na Exaud Mtei(Msaka
Habari)
Wakati wadau mbalimbali
wa maswala ya kisiasa wakipinga kile kinachoendelea visiwani Zanzibar,nao
wajumbe wawili wa tume ya uchaguzi ya Zanzibar ZEC Ndugu NASSOR KHAMIS MOHAMED
na AYOUB HAMAD wameibuika jijini Dar es salaam leo na
kupinga marudio ya uchaguzi unaotaraji kufanyika mwishoni mwa mwezi huu kwa
madai kuwa uchaguzi huo sio halali kulingana na matukio yaliyotokea tangu
kufanyika kwa uchaguzi halali wa October 25 mwaka jana.
Wakizungumza na
wanahabari Jijini Dar es salaam makamishna hao wamesema kuwa sababu kubwa ya
kupinga kufanyika kwa uchaguzi huo ni kutokana na kuvurugwa kwa katiba ya
zanzibar tangu tukio la kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi wa mwaka jana ambapo
wamesema kuwa mwenyekiti wa Tume hiyo hakuwa na mamlaka ya kisheria kufuta
uchaguzi huo bila kuwashirikisha makamishna wa tume hiyo.
Mjumbe wa Tume ya uchaguzi ya Zanzibar NASSOR KHAMIS MOHAMED akizngumza na wanahabari mapema leo Jijini Dar es salaam |
Wamesema kuwa sababu
nyingine inayowafanya kupinga uchaguzi wa marudio ni kutokana na kukamilika kwa
uchaguzi wa mwaka jana ambapo uchaguzi huo ulikuwa umekamilika na baadhi ya
washindi wa viti vya uwakilishi na udiwani walishakabidhiwa vyeti vyao na
mawakala kusaini kuwa uchaguzi huo hauna kasoro hivyo wanashangaa kuambiwa kuwa
uchaguzi huo ulikuwa na kasoro nyingi zilizo pelekea kuubatilisha uchaguzi huo.
Wameongeza kurudiwa kwa
uchaguzi huo ambao unatarajiwa kutumia zaidi ya billion saba hadi kukamilika kwake ni matumizi mabaya
ya rasilimali za taifa kwani uchaguzi Zanzibar ulishafanyika na tayari na
kinachoendelea ni mbinu za kuubatilisha uchaguzi huo.
Wameongeza kuwa tukio
la kufutwa kwa uchaguzi huo lilitanguliwa na matukio kadhaa ambayo yalionyesha
wazi kuwa kuna kikundi cha watu ambacho kinamshauri mwenyekiti wa tume hiyo
JECHA SALUM JECHA na sio maamuzi ya tume nzima.
“Tarehe 26 october
mwaka jana CCM walileta barua ya malalamiko na kumtaka mwenyeikiti na tume
kufuta uchaguzi huo wakati tayari tulishaanza kutoa vyeti kwa washindi,ambapo
mwenyekiti aliitisha kikao cha tume na tulipitisha kwa pamoja kuwa maombi ya
CCM hayakuwa na mashiko hivyo mchakato unaendelea”amesema NASSOR KHAMIS ambaye
ni mmoja wa makishna wa tume hiyo.
Mjumbe mwingine AYOUB HAMAD akifafanua jambo mbale ya wanahabari kuhusu kile kinachoendelea Zanzibar |
Ameendelea kusema kuwa
baada ya maamuzi ya tume ndipo siku iliyofwata mwenyekiti JECHA hakufika katika
ujumuishaji wa matokeo kwa siku nzima na ndipo waliposikia kuwa ametangaza
kufuta uchaguzi bila kuwashirikisha wajumbe wengine wa tume hiyo na baada ya
hapo ndipo ofisi yetu ilianza kuzungukwa na wanajeshi na kuamuriwa tusifanye
lolote huku jaji mkuu wa mahakama ya Zanzibar naye akiwa amekamatwa na kupekwa
polisi.
Wamesema kuwa kwa
matukio kama hayo wanaamini kuwa tume hiyo imeacha kufanya kazi zake kisheria
na sasa inafanya kazi kisiasa jambo ambalo linampotezea sifa mwenyekiti wa ZEC
kuendelea kuiongoza tume hiyo.
Aidha wamesema kuwa
hali iliyopo ndani ya tume kwa sasa sio hali ya kawaidia ambayo inaweza
kusimamia uchaguzi wa haki kwani wajumbe wamekuwa wakipingana kwa kila hoja
inayoletwa jambo ambalo linafanya uchaguzi wa marudio kutiliwa mashaka na
wajumbe wengi wa tume hiyo.
Wajumbe hao wa ZEC
wametoa wito kwa wajumbe wengine ndani ya tume hiyo kuacha kufwata mkumbo na
kuamua kusimamia sheria inavyosema ili kuwapatia wazanzibar haki yao ya
kikatiba
No comments:
Post a Comment