Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi), Dkt. Leonard Chamuriho (kulia), akimkaribisha Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi, Eng. John William Kijazi kwenye Jengo la Ukumbi wa Mikutano la Mwl. Julius Nyerere, wakati alipofika kufungua Mkutano wa siku nne wa kujadili namna ya kuboresha utendaji wa Shirika la Reli la Tanzania na Zambia (TAZARA).Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi, Eng. John WilliamKijazi (kushoto), akisalimiana na ujumbe kutoka Nchini China ambao wanahudhuria Mkutano wa siku nne wa kujadili namna ya kuboresha utendaji wa Shirika la Reli la Tanzania na Zambia (TAZARA) unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano la Mwl. Julius Nyerere. Kushoto kwake ni Balozi wa China NchiniDkt. LU Youqing.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi), Dkt. Leornard Chamuriho (kulia), akitoa hotuba yake kabla ya ufunguzi wa Mkutano wa siku nne wa kujadili namna ya kuboresha utendaji wa Shirika la Reli la Tanzania na Zambia (TAZARA) unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano la Mwl. Julius Nyerere.
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi, Eng. John William Kijazi,akitoa hotuba yake wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa siku nne unaozikutanisha Nchi Tatu China, Tanzania na Zambia kujadili namna ya kuboresha utendaji wa Shirika la Reli la Tanzania na Zambia (TAZARA) unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano la Mwl. Julius Nyerere.
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi, Eng. John William Kijazi (kushoto), akimsiliza Katibu wa Baraza la Mawaziri nchiniZambia, Dkt. Roland Msiska, wakati wakijadili jambo wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa siku nneunazoikutanisha Nchi tatuza China, Tanzania na Zambia kujadili namna ya kuboresha utendaji wa Shirika la Reli la Tanzania na Zambia (TAZARA) unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano la Mwl. Julius Nyerere.
No comments:
Post a Comment