Moja ya mafanikio makubwa ya Chama chochote cha siasa ukiachana na kushika Dola ni kuwa na rasilimali watu ambayo ndiyo chachu kubwa inayowapa nguvu kuyafikia malengo yao kirahisi.
Hivi karibuni chama cha Allience for Democratic Change (ADC) kilitangaza kuanza ziara nchi nzima ambapo walitangaza kuanza na mkoa wa Tanga kwa malengo ya kujitambulisha kwa wakazi wa mkoa huo, kutoa shukrani kwa kura walizopigiwa katika uchaguzi wa Oktoba 2010 na kushika nafasi ya nne kati ya vyama nane, halikadhalika kusajili wanachama wapya.
Katibu Mkuu wa Chama hicho Doyo Hassan Doyo amesema kuwa ziara waliyoifanya siku ya jumamosi mkoani Tanga maeneo ya Mabanda, Misima, Chanika, Konje na Vibaoni ya wilayani Handeni imekuwa ya mafanikio kwao tofauti na matarajio yao.

No comments:
Post a Comment