Na Exaud Mtei
Shirika lisilo la
kiserikali linalojihusisha na maendeleo ya wanawake na jamii kwa ujumla la
WOMEN ACTION TOWARDS ECONOMIC DEVELOPMENT –WATED leo wameendesha majadiliano
maalum na wanasheria mbalimbali nchini kwa lengo la kujadili kwa pamoja dhana
halisi ya maendeleo endelevu ambayo yalizinduliwa na wakuu wa nchi mbalimbali mwaka
jana ambayo moja kati ya malengio yake lengo ka 16 ni maswala ya uhuru wa sheria
na upatikanaji wa sheria katika kuyafikia malengo ya maendeleo endelevu.
Majadiliano hayo
yalilenga kuwawezesha na kujenga uelewa mkubwa kwa wanasheria mbalimbali ili
waweze kutambua wao kama wanasheria wana wajibu gani katika kuwasaidia wananchi
na mtu mmoja mmoja kuweza kuyafikia hayo maendeleo endelevu yanayotajwa katika
malengo hayo.
Imani Kaduma moja kati ya wanasheria waliopata nafasi ya kutoa michango yao leo |
Mariam Matui ni katibu
wa shirika la WATED Tanzania na anaeleza kuwa sababu kubwa ya kuamua kufanya
majadiliano hayo ni kutokana na ukweli kwamba bado kuna haja kubwa ya kuhusisha
jamii hususani wanasheria waweze kufahamu kwa kina malengo hayo kwakuwa
wanasheria ndio wanaosaini na kuandika na kuandaa mikataba mbalimbali hivyo kama wanasheria
wakiwa na uwezo wa kuyadadavua kwa kina hayo maendeleo endelevu itasaidia nchi
zetu hususani Tanzania kuweza kuyafikia maendeleo hayo.
Damas Ndumbaro akichangia katika mjadala huo |
Imani Kaduma ni moja
kati ya wanasheria ambao walipata nafasi ya kuchagia mawazo yake katika mjadala
huo uliofanyika Jijini Dar es salaam ambapo katika mchango wake ameeleza kuwa
pamoja na Tanzania kuonekana kuwa ina mifumo mizuri ya kutufikisha katika
malengo hayo ya maendeleo endelevu lakini bado chagamoto kubwa imebaki katika
swala la uongozi ambapo swala la matumizi mabaya ya madaraka limekuwa moja kati
ya vizuizi vikubwa katika mataifa mengo barani Africa likiwemo Tanzania ya
kuyafikia malengo hayo.
Dr GILES DZOUSA NI MTAALAM WA GOVERNANCE KATIKA ARDHI |
Sakata la rushwa pia
limetajwa kama moja kati ya mambo yanayorudisha nyuma juhudi za kuyafikia
malengo ya maendeleo endelevu katika mataifa mengi ya kiafrika.Mwanasheria
mkongwe nchini DR DAMAS NDUMBARO ameeleza kuwa nchini Tanzania maswala kama
migogoro ya ardhi katika vijiji mbalimbali imekuwa ikichangiwa kwa kiasi
kukubwa na maswala ya rushwa ambapo
pamoja na viongozi wa vijiji kujua kuwa wanawahujumu wananchi wamekuwa
wakirubuniwa kwa pesa na wageni na kujikuta wakiwauzia maendeo ya vijiji ambayo
mwishoni huzua migogoro mikubwa na isiyokwisha.
Mshauri wa serikali ya Tanzania kutoka umoja wa mataifa UN Dr CHITRALEKHA MASSEY akichangia jambo katika majadilinao hayo |
Katika majadiliano hayo
yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ubalozi wa Uingereza Jijini Dar es
salaam yaliwakutanisha wadau mbalimbali wa maswala ya kisheria wakiwemo
washauri wan chi kutoka Umoja wa mataifa,wanasheria wenye uzoefu pamoja na
viongozi wa shirika hilo..PICHA NYINGINE ZA TUKIO HILO UNAWEZA KUENDELEA CHINI.asante
No comments:
Post a Comment