Sheikh HEMED JALALA akizungumza na wanahabari Wakati wa maadhimisho ya siku ya QUDS ndani ya msikiti wa kigogo Post Dar es salaam(PICHA STORY NA EXAUD MTEIMSAKA HABARI) |
Wakati wauminiwa dini
ya kiislam duniani na nchini Tanzania wakiendelea
na mfungo wa mwezi mtukufu wa ramadhani wito umetolewa kwa viongozi wa kidini
pamoja na vyombo vya umoja wa mataifa kuhakikisha
kuwa wanarudisha hali ya Amani katika nchi ya palestina ambayo wananchi wake
wamekuwa wakiishi katika mateso,dhuluma na hali ngumu kutoka kwa nchi ya Israeli
na kuwafanya wananchi wa palestina kushindwa kufurahia kuishi katika nchi yao.
Wito huo umetolewa na Kiongozi Mkuu wa Dhehebu la Shia nchini Tanzania kutoka msikiti wa kigogo post
uliopo Jijini Dar es salaam Sheikh HEMED JALALA wakati wakiwa katika
maadhimisho ya siku ya QUADS duniani ambayo ni siku inayotumika kuwakumbuka na
kutafakari kwa pamoja mateso na mambo mbaya wanayopitia wananchi wa palestina.
Baadhi ya waumini wa dini ya kislam wakipata semina juu ya siku hiyo ya QUDS katika msikiti wa Kigogo Post Dar es salaam |
Akizungumza na
wanahabari Sheiokh JALALA amesema kuwa wapalestina wamezagaaa duniani kwa
kufukuzwa katika nchi yao na kuishi kwa mateso ambapo amesema kuwa wao kama
waislam hawawezi kukubali uvamizi kama huu kwa watu ambao hawana hatia hivyo
wanaomba vyombo vinavyohusika vikiwemo vile vya umoja wa mataifa kuhakikisha
wanarudisha Amani kama iliyopo Tanzania kwani uwezo wa kufanya hivyo upo.
Ameeleza kuwa kwa umtu
ambaye anatambua historia ya nchi hiyo ya palestina na mambo yanayopitia ni
dhuluma,ukandamizaji,na matesho makubwa jambo ambalo halifai kunyamaziwa,huku
akisema kuwa ni ukweli kwamba mambo ya palestina ni ya wapalestina ila kwa sasa
palestina haipo mikononi mwa wapalestina jambo ambalo linawapa nguvu wao
kuinuka na kupiga kelele juu ya wanadamu hao wanaoteseka bila hatia.
Itakumbukwa kuwa
mgogoro wa nchi hizo mbili kati ya Israel na palestina umekuwa wa muda mrefu
huku ukisahaulika ambapo wananchi wa palestina wamekuwa wakikumbana na matesho
makubwa kutoka kwa majeshi ya Israel na hata wengine kuikimbia nchi hiyo
kutokana na mateso hayo jambo ambalo limekuwa likiwanyanyua vinywa viongozi wa
dini mbalimbali akiwemo Sheikh JALALA kulaani matesho hayo nayaoendelea nchini
palestina.
AUDIO YA STORY HII IPO HAPO
AUDIO YA STORY HII IPO HAPO
No comments:
Post a Comment