Na
Exaud Mtei (Dar es salaam)
Wakati
report za mateso na dhuluma zikiendelea kurepotiwa duniani zikiyahusisha
mataifa ya pelestina na israel ambapo taarifa zimekuwa zikendelea kuonyesha
jinsi Taifa la palestina wananchi wake wanavyopata mateso kutoka kwa taifa la
israeli hatimaye Kiongozi Mkuu wa kiroho wa Waislam Dhehebu la SHIA ITHNASHERIYA Tanzania Sheikh HEMED JALALA ameibuka na kuvitaka vyombo
husika vikimeno umoja wa nchi za ulaya,umoja wa nchi za Africa,umoja wa nchi za
kiarabu na dunia nzima kwa ujumla kuonyesha dhamira ya dhati ya kulisaidia Taifa
la palestina na kuondokana na mateso wanayoyapata kutoka kwa taifa la Israeli mateso
ambayo yamekuwa yakiendelea kwa miaka
mingi sasa.
Sheikh
JALALA akizungumza na wanahabari mapema leo Jijini Dar es salaam ikiwa ni
kuelekea uazimisha siku ya QUDS duniani ambayo ni siku maalum ya kukumbuka
mateso wanayokumbana nayo wananchi wa palestina amesema kuwa imefikia wakati
sasa dunia kwa pamoja kuungana bila kujali Dini na itikadi zake na kupigania
haki ya wapalestina kwani wanaoteseka kule sio waislam pekee bali ni wananchi
wote na hata wale wasio na dini.
Akieleza
sakata linaloendelea katika nchi hiyo ya palestina amesema kuwa mateso yamekuwa
yakiongezeka kadiri siku zinavyosogea ikiwa ni pamoja na nyumba za wananchi
kuvunjwa,makanisa na misikiti kuharibiwa,mauaji ya kila kona,na kuharibiwa kwa
mashamba yao ambayo wamekuwa wakulima wa mazao ya mizaituni jambo ambalo
amesema kuwa linaonyesha wazi ni mipango ya wazi ya kuwamaliza wapalestina na
kuwaondoa kabisa katika ardhi yao jambo ambalo amesema halifai kunyamaziwa na
walimwengu wote.
Ameogeza
kuwa mkakati uliopo hapo kwa sasa ni mkakati wa kufutwa kabisa kwa upalestina
na kuwaondoa kabisa katika ardhi yao na katika nchi yao wakati ni wazi kwa nchi
hiyo ni nchi yao halali na wanastahili kuishi kwa Amani kama mataifa mengine.
Akielezea
jinsi dunia inavyotakiwa kuungana amesema kuwa katika kuwapigania wapelestina
waweze kupata Amani yao sio maswala ya kidini wala kiitikadi bali ni jambo la
kibinadamu ambalo halina dini wala kabila na ni jambo la utu la kutetea haki za
wanadamu wenzetu ambao wanateseka mikononi mwa waisrael.
Pamoja
na wito huo na kilio cha SHEIK JALALA pia ametoa wito kwa watanzania wote
wakiwemo viongozi wan chi kutokana na
historia nzuri iliyopo tangu kipindi cha baba wa Taifa Mwalimu NYERERE la kuwa taifa
lenye mahusiano mazuri kwa wapalestina
amelitaka taifa kufwata nyayo za Baba wa taifa na kuamua kuwasemea wapalestina
na kuhakikisha kuwa wanapata haki yao wanayostahili.
Katika
kuonyesha kukerwa na maswala yanayoendelea nchini palestina Sheikh JALALA
amewataka watanzania wote kwa ujumla kutoka kwa umoja wao siku ya ijumaa ya
tarehe 1,mwezi wa Saba kufanya matembezi ya Amani ya kuonyesha dunia kuwa
watanzania tunapinga kwa pamoja dhuluma wanayofanyiwa wapalestina katika ardhi
yao matembezi ambayo yatafanyika katika Jiji la Dar es salaam.
Mgogoro
wa Mataifa ya palestina na Irael ni mgogoro mkubwa ambao kwa sasa umechukua
miaka mingi na umekuwa ukikuwa mwaka hadi mwaka huku taifa la palestina likionekana
kuumizwa Zaidi na mgogoro huo kutokana na madhara makubwa yanayowakumba
wananchi wake likiwemo wananchi kuuawa,wengine kukosa makazi pamoja na maelefu
ya wananchi wa palestina kufungwa katika magereza ya Israeli kwa sababu ambazo
sheikh JALALA amezitaja kuwa hazina mashiko.
No comments:
Post a Comment