NI
kampuni inayojihusisha na kuendeleza biashara za wanawake wajasilia mali wa
tanzania. TWCC ni shirika lisilotengeneza faida na fedha inayopatikana
uzungushwa na higaiwa kama gawio. Pia inajihusisha na vitu vingi kama kutoa
mafunzo ya kibiashara kwa wanawake wote,pia wanatumia kuwajengea uwezo wa
kutumia mikopo mbalimbali ili kuweza kuendesha biashara zao, kuwapeleka sehemu
mbalimbali za maonyesho kama saba saba nane nane na matamasha ya kimataifa ili
kuweza kujifunza ushindani wa kibiashara,pia wanasidia wanawake wote hata kama
sio wanachama ila kwa upande wa fursa zinatolewa kwa wanachamma kwanza.
TWCC inashirikiana na mashirika mbalimbali ya kiserikali na
yasiyo ya kiselikali ili kuweza kupata misaada mbalimbali baadhi ya mashirika
hayo ni kama UN woman,CRDB, MNB pamoja na wizara mbalimbali kama vizara ya
viwanda na biashara pamoja na wizara inayojihusisha na wanawake.
Ndani ya banda lao lililopo sabasaba kuna mkusanyiko wa wafanya
biashara toka mikoa mbalimbali kama, Moshi Arusha Tanga Dar es salaam na mikoa
mingine wanachama,na wote wamekuja na biashara tofauti tofauti ikiwa ni kazi za
mikono yao wenyewe na baadhi ya bidhaa hizo ni sabuni, dawa za madoa,batiki,
mikeka, na bidhaa nyingine nyingi ikiwemo nafaka.
Akizungumza na mwandishi wa Mtandao huu ambao umeweka kambi
katika maonyesho ya saba saba Jijini Dar es salaam amesema kuwa Changamoto
kubwa walio nayo ni fedha kampuni inakuwa na wakati mgumu kwa kuwa kwenye
maonyesho kama hayo inabidi iwafadhili toka mikoa wanayotoka mpaka hapa walipo
na pia kuwafundisha pamoja na kuendesha semina jinsi ya kuwasaidia wanawake
wengi zaidi na kitu kingine ni kukosa masoko ya uhakika kwa ajili ya wajasilia
mali hao.
TWCC inawashauri wanawake Tanzania kuweza kujiunga ili kuweza kusaidiwa kujipeleka
mbele Zaidi pia inawashauri mabinti wadogo kuja kwa wingi na kuachana na dhima
ya kuajiriwa ni bora waweze kujiunga huku ili kutimiza ndoto zao. hao yote
yamesemwa na MWAJUMA HAMZA Deputy executive director wa TWCC. na anawashuri
watanzania wote kuweza kutembelea banda lao lililopo karibu na wizara ya mali
asili na utalii kwa kuweza kuwaunga mkono wakina mama wa kitanzania ili kuweza
kuwapa uwezo wa kutangaza soko la nyumbani
No comments:
Post a Comment