Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania
(TFF), Jamal Malinzi amewatakia kila la kheri Waislamu wote nchini katika
kipindi cha Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani unaoanza sasa.
Rais Malinzi amewataka Watanzania
kuendeleza tunu za amani na utulivu ili kushiriki katika ibada kama
inavyostahili. Amesema kufanikiwa wa Waislamu katika ibada hiyo ni chachu ya
mafanikio ya kila sekta na hasa soka ambalo hupendwa na mashabiki wengi ndani
na nje ya nchi.
No comments:
Post a Comment