The mboni show yawafuturisha watoto Yatima Dar,Makamu wa Rais Mama Samia awapongeza
Kipindi cha The Mboni Show, chini ya Mtangazaji wake, Mboni Masimba ambacho kinachorushwa kupitia televisheni ya Taifa ya TBC, Jioni ya jana ya Juni 29.2016 wameweza kufuturisha wageni Watoto Yatima 268 kutoka katika baadhi ya vituo vya Mkoa wa Dar es Salaam kwa lengo la kuwafariji na kuwasaidia kama ilivyo kwa desturi ya waandaaji wa kipindi hicho huku Mama mgeni rasmi akiwa Makamu wa Rais Mama Samia Hassan Suluhu.
Akizungumza katika tukio hilo mara baada ya kufuturisha Watoto hao pamoja na wageni mbalimbali Mwanadada Mboni ameeleza kuwa, wamekuwa wakifanya hivyo mara kwa mara hii ni kutokana na kurudisha fadhila kwa jamii kwa kidogo kinachopatikana hivyo amewaomba wadau wengine kujitokeza kufanya jambo kama hilo kila inapohitajika kwa jamii.
Kwa upande wake, Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu amepongeza tukio hilo la Mwanadad Mboni Masimba kwani ni la kuigwa hivyo ni lazima jamii imuunge mkono kwa kujilea kwake.
"Nakupongeza Mboni na timu yako kwa kuwakumbuka watoto hawa. Tukio kama hili kuliandaa linahitaji gharama na kujitolea haswa. Tupo pamoja nawe na juhudi zako tunaziona nakupongeza sana." alibainisha Makamu wa Rais Mama Samia.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mh. Paul Makonda, alimpongeza Mboni Masimba kwa shughuli hiyo kwani inasadia katika kukumbuka jamii hasa watoto hao ambao wengi wao wanalelewa katika vituo vya Yatima.
Katika tukio hilo lililofanyika katika ukumbi wa Karimjee uliopo Posta jijni Dar es Salaam mbali na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh. Paul Makonda, Pia viongozi wengine kadhaa walijumuika akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Kinondoni, Mh Ali Hapi na viongozi wa dini Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Mussa Salum pamoja na Kaimu Mufti wa Tanzania aliyemwakilisha Mufti Mkuu pamoja na Mabalozi akiwemo Balozi wa INDIA.
Pia wadau wa kipindi hicho cha The Mboni Show, watu maarufu, Wasanii, Wanahabari na wadau wengine wakiwemo wadhamini waliofanikisha shughuli hiyo.
Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu akiwasili kwenye tukio hilo la la kufuturisha watoto zaidi ya 268 lililoandaliwa na Mwanadada Mboni Masimba (kulia) anayeendesha kipindi cha The Mboni Show, kupitia televisheni ya TBC. Tukio hilo limefanyika jioni ya Juni 29.2016 katika viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wadau wakiwasilia kwenye tukio hilo kumpa kampani Mwanadada Mboni Masimba
Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa katika tukio hilo
Meza kuu, Mama yake Mzazi, Mboni Masimba( kushoto), Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu na Mboni Masimba wakifuatilia tukio hilo
Meza kuu : Mufti Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Makamu Mufti wa Tanzania na Mkuu wa Mkoa wa Dar
Baadhi ya watoto kutoka katika vituo vya kulea watoto Yatima ambao waliandaliwa futari hiyo maalum wakiwa katika tukio hilo
Mmoja wa wasomaji wa dini ya kiislamu akiendelea na dua
baadhi ya watoto walioandaliwa shughuli hiyo
Wageni waalikwa wakiwa katika shughulo hiyo
Wadau
Dua zikiendelea
Mkuu wa Mkoa wa Kinondoni, Mh. Ali Hapi akipata futari hiyo
Mwanadada Mboni Masimba akizungumza machache kuhusiana na tukio hilo
Mwakilishi wa Mufti Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar, Mh. Makonda
Baadhi ya wageni waalikwa wakiwemo Mabalozi
Mkuu wa Mkoa akiagana na wadau katika tukio hilo
Wadau waliojitokeza kumuunga mkono Mwanadada Mboni Masimba
Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu ( wa tatu kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mboni Mboni Masimba, Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam (kulia). Wengine ni Mama Mazazi wa Mboni Masimba, akifuatiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mh. Makonda na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ali Hapi. Wakati wa tukio hilo la kufuturisha watoto zaidi ya 268 lililoandaliwa na Mwanadada Mboni Masimba wa kipindi cha The Mboni Show, kupitia televisheni ya TBC. Tukio hilo limefanyika jioni ya Juni 29.2016 katika viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Andrew Chale, Modewjiblo
No comments:
Post a Comment