Katibu wa Itikadi mawasiliano na uenezi wa chama cha ACT WAZALENDO Ndugu ADO SHAIBU akizngumza na wanahabari leo Jijini Dar es salaam kuhusu mapokezi ya kumpokea kiongozi yao na mbunge pekee wa chama hicho ZITTO KABWE ambaye naye amekumbwa na timua timua ya bungeni,mapokezi ambayo yatafanyika Jijini Dar es salaam siku ya Jumapili Na EXAUD MTEI |
Story ambayo bado ipo
maskioni mwa watanzania walio wengi ni mwenendo wa bunge la Jamhuri ya muungano
wa Tanzania na mizengwe yake ambayo imesababisha wabunge saba wa vyama vya upinzani
kusimamiswa kushiriki shughuli za bunge kwa vipindi Tofauti tofauti akiwemo mbunge
kutoka ndani ya chama cha Act wazalendo Mh ZITTO ZUBERI KABWE na wabunge wa
vyama vya UKAWA.
Sakata hilo limeendelea
kuchukua Headline katika maeneo mbalimbali ambapo asubuhi hii chama cha ACT
wazalendo kupitia kwa kiongozi wao ADO SHAIBU wamejitokeza mbele ya wanahabari kueleza
msimamo wa chama chao kuhusu sakata hilo.
Akizungumza na wanahabari
leo Katibu huyo wa itikadi mawasiliano na uenezi wa ACT ADO SHAIBU ameeleza
kuwa chama hicho kimeandaa mapokezi ya kiongozi wao ambaye amekumbwa na adhabu
hiyo mapokezi ambayo yanataraji kufanyika Jijini Dar es salaam na baadae
kufwatiwa na mkutano mkubwa wa hadhara ambao umepangwa kufanyika katika viwanja
vya ZAKIEM mbagala lengo likiwa ni kuwapa nafasi wabunge hao kueleza ukweli wa yale
yanayoendelea bungeni Dodoma.
Pamoja na mandalizi
hayo chama hicho kimewaandikia barua makatibu wa vyama vya upinzani ambao nao
wanapinga adhabu hiyo kutoka CHADEMA,CUF,na NCCR-MAGEUZI kuwaomba kuungana nao
katika mapokezi hayo ambayo yamepewa jina la OPERATION LINDA DEMOCRASIA na bado
hawajapata majibu yao lakini wanaamini wataungana nao katika Operation iyo
ambayo itafwatiwa na mikoa mingine takribani minne.
Habari24 tv imekuwekea
video ya mkutano huo wa wanahabari leo asubuhi
No comments:
Post a Comment