Na Vicent Macha-Dar
es-salaam
Wakati ikiwa ni siku
moja baada ya bajeti ya Tanzania kwa mwaka 2016/2017 ikiwa imesomwa na kuanza
kujadiliwa Bungeni wadau mbalimbali wameanza kutoa maoni kuhusu bajeti hiyo ambapo
wanaharakati mbalimbali wakiongozwa na mtandao wa jinsia TGNP wakipinga vikali
bajeti hiyo kwa kile wanachodai kuwa bajeti hiyo imelenga Zaidi kwa secta
binafsi na wafanyabiashara na kuwasahau wananchi wa kawaida ambao ni
wazalishaji wakuwa na walipa kodi wakubwa.
Akizungumza na
wanahabari leo Jijini Dar es salaam mwenyekiti wa vituo vya taarifa na maarifa
Taifa ambaye pia ni mwenyekiti maarifa wa kata ya makumbusho Bi JANETH MAWIZA amesema
kuwa vipaumbele ambavyo vimewekwa kwa bajeti ya mwaka huu ni wazi kuwa havimlengi
mtu wa pembezoni na badala yake vinawalenga wawekezaji wakubwa na kuwaacha
masikini pembeni ambapo ameeleza kuwa kutokjana na hali hiyo haitamuwezesha
mtanzania masikini kuwa na masha bora hata kama uchumi nutakuwa
Ameongeza kuwa bajeti
ya mwaka huu iliyosomwa jana bungeni Jana
wao kama wanaharakati wanadai uwajibikaji wa serikali katika kusimamia
ukusanyaji wa mapato na kutafuta vyanzo mbadala vya mapato endelevu ili
kudhibiti kuendelea kukopa.
Mwenyekiti wa vituo vya taarifa na maarifa Taifa ambaye pia ni mwenyekiti maarifa wa kata ya makumbusho Bi JANETH MAWIZAakisoma Tamko la wanaharakati hao juu ya Bajeti ya nchi Iliyosomwa jana Bungeni Dodoma na Kugusa Hisia za watanzania wengi. |
Aidha mambo mengine ambayo
wanaharakati hao wanadai ni pamoja na kuwepo mfumo shirikishi na endelevu
katika kutengeneza na kufwatilia utekelezaji wa bajeti.kuongezwa kwa bajeti ya
maji,na afya ambazo wamedai ni ndogo sana na haziwezi kutimiza malengo mazuri
hasa kwa wanawake wa Tanzania.
Nimekuwekea Video
Kuhusu Tukio hilo
No comments:
Post a Comment