Mama ANNA MGWIRA mwenyekiti wa chama hicho akizungumza na wanahabari dakika chache zilizopita katika ofisi za makao makuu ya chama hicho |
Kongamano lililokuwa
limeandaliwa na cham cha kisiasa cha ACT WAZALENDO chini ya kiongozi wake mkuu
ZITTO KABWE limeshinda kufanyika baada ya watu wanaodhaniwa ni polisi kuzuia
kongamano hili bila kutoa sababu yoyote kwa wandaaji hao.
Kongamano hilo ambalo
lilitakiwa kuanza leo siku ya juumapili saa saba mchana katika ukumbi wa LAPF millennium
Tower Dar es salaam limeshindwa kufanyika kutokana na Askari waliokuwa
wametanda nje ya ukumbi huo wakiwazuia wanachama na wadau mbalimbali waliokuwa
wamealikwa katika kongamano hilo.
Akizungmza na
wanajanari muda mfupi baada ya Kuzuiwa kwa kongamano hilo mwenyekiti wa ACT
WAZALENDO Mama ANNA MGWIRA amesema kuwa taarifa za kuziuwa kwao wamezipata
kutoka kwa mmiliki wa ukumbi huo ambapo amewaambia kuwa Wamepigiwa simu na
askari kuwa wasiruhusu kufanyika kwa kongamano hilo kinyume na hivyo
wangefungiwa biashara yao hiyo.
Ameendelea kusema kuwa
waliambiwa na mmiliki wa ukumbi huo kuwa askari walianza kutanda nje ya ukumbi
huo tangu saa 12 asubuhi jambo lililoashiria kuwa kongamano hilo halitafanyika.
MGWIRA amesema kuwa wao
kama chama wameshtushwa sana na taarifa hizo ambazo hata walipompigia kamanda
wa polisi mkoa amesema kuwa hana taarifa za kuzuiwa kwa kongamano hilo jambo
ambalo linawapa mashaka kuwa ni nani anafanya mambo hayo ambayo yanarudisha
nyuma democrasia.
Baada ya kuzuiwa sasa
chama hicho kimetangaza kuwa kitakutana kwa dharura na kujadili hali
inayokikumba chama hicho ikiwa ni wiki mojua tuu kwa kiongozi wao ZITTO KABWE
kuhojiwa na njeshi la polisi kuhusu kauli zake juu ya Rais katika mkutano wake
wa mbagala.
Kongamano hilo awali
lilielezwa kuwa ni kwa ajili ya kujadili maswala muuuhimu ya Bajeti na kumpa
nafasi kiongozi wao huyo kutoa maoni yake juu ya bajeti ya mwaka huu kwa kuwa hawezi
kuyatoa bungeni kutokana na kusimamishwa kwake kuhudhuria vikao vya bunge
No comments:
Post a Comment