Makamu wa Raisi Mama Samia
Suluhu Hassani siku ya jana aliweza kutembelea banda la chama cha wafanya
biashara wanawake Tanzania TWCC aliweza kupongeza jitihada mbalimbali zinazofanywa
na wanawake hao huku akieleza kuvutiwa
sana na bidhaa za ngozi kama viatu vya aina mbali mbali kama viatu na mikoba ya
kina mama inayotengenezwa kwa ngozi inayopatikana hapa hapa na aliweza
kuwapongeza wafanyabiashara wotewanaopatikana ndani ya banda la TWCC ikiwa ni
mafanikio makubwa kwa chama hicho kwa mara ya kwanza kuweza kuwa na banda lake
lenyewe.
Pia mama Samia ameweza
kuwasifu sana TWCC kwa kuweza kuanzisha majukwaa mbalimbali ikiwa kwa sasa
chama hicho kina majukwaa 11 katika mikoa 9 ikiwa ni jitihada za kuwasidia
wanawake wengi zaidi na pia aliweza kuvutiwa baada ya kuona wanawake walemavu
wakipewa nafasi katika chama hicho na aliweza kuwashauri watengenezaji wa
bidhaa za ngozi kuwa waweze kufanya finishing vizuri kwa kuwa bidhaa zao ni
nzuri na zinaweza kuuzika hata nje ya mipaka ya Tanzania.
Na kutokanana na
changamoto ya kutopatikana kwa soli na mashine nzuri za kufanyia kazi hapa
nchini mpaka kuweza kuagiza nchi za nje waziri wa viwanda na biashara alisema swala
limeshafika kwenya wizara yake na watalifanyia kazi alisema kutokana selikali
ya awamu ya nne ni ya viwanda basi itahakikisha inasaidia viwanda vidogo vidogo
viweze kuwa na nguvu kubwa ili bidhaa zetu ziweze kuuzika kimataifa na kutanua
wigo kwa wajasilia mali wadogo wadogo.
Catheline Chitinde ni
mmoja wa wafanya biashara ndani ya banda la TWCC ambae yeye ni anahusika na bidhaa
zitokanazo na ngozi anasema amefurahi sana baada ya kutembelewa na Makamu wa Raisi
na yeye anaamini tatizo lao linalowasumbua la kutopatikana kwa soli litaisha.
Aidha anasema wanachokiomba kwa serikali ni kuweza
kupata maeneo ya kuuzia bidhaa zao yaani serikali ingetenga maeneo rasmi
kwaajili ya kuuza bidhaa zinazotengenezwa na wajasilia mali kutoka Tanzania.
No comments:
Post a Comment