Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kesho Jumamosi Julai 30, 2016 anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa mashindano ya kuibua na kukuza vipaji vya mpira wa miguu kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume ulioko kwenye makutano ya Barabara za Uhuru na Shaurimoyo, Ilala jijini Dar es Salaam.
Sambamba na Makonda, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi naye amethibitisha kuwako kwenye hafla hiyo ambayo mchezo wa kwanza utazikutanisha timu za Ilala Boys dhidi ya Bombom Ilala, Dar es Salaam. Inawakilishwa na mikoa yote mitatu kisoka ambayo ni Ilala, Kinondoni na Temeke kwa pande zote mbili za wavulana na wasichana.
Kadhalika, wakuu wa mikoa mingine ambayo mashindano hayo yatafanyika nao watakuwa wageni rasmi katika mikoa yao ambayo ni Mbeya, Mwanza na Morogoro kwa upande wa wavulana pia Arusha, Lindi na Zanzibar kwa upande wa wasichana.
No comments:
Post a Comment