Chama
Cha Waandishi wa Habari za Michezo (TASWA),kimepokea kwa masikitiko
makubwa taarifa za msiba wa mwanachama wake,Elizaberth Mayemba
kilichotokea jana jioni huko nyumbani kwake Tabata kwa Swai.
TASWA
imestushwa na kuhuzunishwa sana kutokana na kifo hiki cha Elizaberth
ambaye mchango wake katika tasnia ya habari za michezo bado ulikuwa
unahitajika sana.
Waandishi
wa Habari za michezo wataendelea kumkumbuka Elizaberth kutokana na
ucheshi,kujituma na uwajibikaji katika kufanikisha kazi zake na kuwa
mfano kwa waandishi chipukizi.
TASWA
inatoa pole kwa familia ya marehemu, marafiki na waandishi wote wa
habari na kuwatakia moyo wa subira katika wakati huu wa majonzi ya
kuondokewa na mpendwa wetu.
Mwenyezi
Mungu aipumzishe mahala pema peponi roho ya marehemu. TASWA ipo pamoja
na familia ya marehemu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.
Juma Pinto
Mwemyekiti TASWA
|
No comments:
Post a Comment