Sunday, July 31, 2016

WAZIRI NAPE,LOWASA,MBOWE WAWAONGOZA WANAHABARI KUMUAGA MWANDISHI SENGA

S1Wapiga picha wakibeba jeneza la marehemu Joseph Senga aliyekuwa mpiga picha wa gazeti la Tanzania Daima ili  kuliweka kwenye tayari kwa safari ya kwenda Wilayani Kwimba  Mkoani Mwanza kwa mazishi wanaoongoza mbele katikati ni Rafiki yake Mkubwa Deus Mhagale Mpiga picha wa Gazeti la Mtanzania aliyeshika Msalaba , kulia aliyeshika Shada la maua ni John Bukuku mpigapicha na  Mkurugenzi wa Blog ya Fullshangwe  na  kushoto aliyeshika picha ya marehemu  ni Joachim Mushi mpiga picha na Mkurugenzi wa Mtandao wa The Habari akiwa pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mablogger Tanzania TBN wakati wa shughuli ya kuaga mwili wa Marehemu Sinza jijini Dar es salaam.
S2Deus Mhagale Mpiga picha wa Gazeti la Mtanzania kulia Mpiga Picha Loveness aliyekuwa mfanyakazi mwenzake na marehemu kwenye kampuni ya Free Media inayoendesha gazeti la Tanzania Daima na Mpiga Picha Halima Kambi kutoka Guardian  wakiwa wamebeba mashada ya maua na msalama.
S3S4Deus Mhagale Mpiga picha wa Gazeti la Mtanzania akiaga mwili wa marehemu Joseph Senga na kushoto ni Mpiga Picha mkongwe Juma Dihule.
S5
Carthubert Kajuna Mpiga Picha na Mkurugenzi wa Blogu ya Habari na Matukio akiaga mwili wa marehemu Joseph Senga.
S6
Mpiga Picha wa Gazeti la Habari leo Robert Okanda akiaga mwili wa marememu.
S7
Mpiga picha Muhidin Sufiani akitoa hesgima zake za mwisho kwa marehemu Joseph Senga.
S8
Baadhi ya wapiga picha wakijadiliana mambo kadhaa.
S9S10
Mpiga Picha wa Jambo Leo Dotto Mwaibale akitoa heshima za mwisho kwa marehemu Joseph Senga.
S11
Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowasa akiongozana na Nape Nnauye Waziri wa habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kutoa heshima za mwisho kwa marehemu Joseph Senga.
S12
Waziri Mkuu wa Zamani Edward Lowasa akijadiliana jambo na Nape Nnauye Waziri wa Habari , Utamaduni , Sanaa na Michezo wakati walipoongoza waombolezaji katika kuaga mwili  wa mwanahabari Marehemu Joseph Senga
S13

No comments: