Kaimu
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Shaka
Hamdu Shaka akiwaonesha Waandishi wa habari barua walioiandikia Jeshi la
Polisi kuomba kibali na Ulinzi cha kufanya Maandamano hayo ya
amani,wanayotarajia kufanya Agosti 31,kwa minajili ya kumpongeza na
kueleza Wananchi utendaji kazi wa Rais Dkt John Pombe Magufuli.
Kaimu
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Shaka
Hamdu Shaka akitoa ufafanuzi kwa baadho ya maswali mbalimbali yaliyokuwa
yakiulizwa na Waandishi wa habari kuhusiana na Maandamano hayo ya amani
yanayotarajiwa kufanyika Agosti 31,kwa minajili ya kumpongeza na
kueleza Wananchi utendaji kazi wa Rais Dkt John Pombe Magufuli.
Kaimu
Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Shaka
Hamdu Shaka akizungumza na Waandishi wa habari Makao makuu ya Ofisi hizo
mapema leo jijini Dar kuhusiana na kufanya maandamano ya amani Agosti
31,kwa minajili ya kumpongeza na kueleza Wananchi utendaji kazi wa Rais
Dkt John Pombe Magufuli.PICHA NA MICHUZI JR.
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Umoja
wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) wanatarajia kufanya maandamano
ya Amani Agosti 31 kwa ajili ya kueleza utendaji kazi wa Rais Dk.John
Pombe Magufuli kwa Watanzania.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam,Kaimu Katibu Mkuu wa
Umoja huo, Shaka Hamdu Shaka amesema kuwa maandamano hayo
wameshamwandikia barua mkuu wa jeshi la Polisi kwa ajili ya kupata
ulinzi siku hiyo’
Amesema
kuwa wasipopata ulinzi watafanya kwa kujilinda wenyewe ikiwa ni lengo
la kufikisha ujumbe kwa wananchi juu ya utendaji kazi wa Rais Dk. John
Pombe Magufuli.Shaka amesema kuwa Rais Dk.John Pombe Magufuli amefanya
watendaji kuwa na utii pamoja na maadili katika utoaji wa huduma kwa
wananchi.
Aidha
amesema kuwa maandamano hayo wanaawalika na vijana wa vyama vingine
kushiriki kwa lengo moja tuu,la kuunga mkono utendaji wa Rais Dkt.John
Pombe Magufuli.
Shaka
ameongeza kuwa hawana nia mbaya katika maandamano, “kiu yetu kutaka
kufikisha ujumbe kwa wananchi juu ya Rais anachokifanya katika kuwaletea
huduma na Maendeleo Watanzania”,alisema Shaka.
No comments:
Post a Comment