Kampuni ya PURPLE COW
MEDIA LTD ya nchini Tanzania leo imeta ngaza rasmi kuzindua kwa Tamasha kubwa
Jijini Dar es salaam lililopewa Jina la PAMOJA CARNIVAL litakalofanyika katika
viwanja vya Leaders Club kinondoni tamasha ambalo lina lengo la kuwaleta watu
pamoja na kujifunza Njia Rahisi namna ya kijilinda na kuepuka ajali za
Barabarani pamoja na kuburudika.
ANTONY KIZITO ambaye ni meneja masoko wa Quality Group ambao ni moja ya wafanikishaji wa Tamasha hilo akieleza mipango ya kufanikisha Tamasha Hilo. |
Akizungumza na Wanahabari
Jijini Dar es salaam Leo wakati wa kuzindua Tamasha hilo ANTONY KIZITO ambaye
ni meneja masoko wa Quality Group ambao ni moja ya wafanikishaji wa Tamasha
hilo amesema kuwa Tamasha hilo litafanyika tarehe 24 mwezi wa tisa mwaka 2016
ambapo watanzania watapata nafasi ya burudani na michezo mbalimbali,kushiriki
kwenye maonyesho ya vipaji,ubunifu pamoja na biashara mbalimbali za
wajasiriamali makampuni mbalimbali huku pia wananchi wakipata nyama choma na
vyakula mbalimbali vya kiasili vilivyoandaliwa na wasanii wakubwa nchini hii
ikiwa ni njia ya kuwahimiza kuwa Tanzania yenye neema bila ajali za hovyo
inawezekana.
Bei Ya Viingilio unaweza kutizama hapo |
Kizito ameongeza kuwa sababu
kubwa ya lengo lao ni kutokana na ukweli kuwa ajali za barabaranbi zimekuwa
zikiongezeka kila kukicha nchini Tanzania na kila mtanzania amekuwa akiguswa na
madhara ya ajali hizo ikiwemo kupoteza ndugu na jamaa au marafiki,kupata
ulemavu na hata uharibifu mkubwa wa mali hivyo tamasha hilo linatumika kuwaleta
watanzania pamoja na kujua mbinu mbalimbali za kujikinga na madhara hayo.
Maswala mengine ambayo
watanzania watapata kujifunza ni pamoja na matatizo yanayotokea kwenye aina za
usafiri mbalimbali yakiwemo kusahau mizigo kwenye usafiri,ajali za kizembe,na
kuporwa wakati wakusafiri ambapo katika tamasha hilo kutakuwa na makampuni
mbalimbali ambayo yatatoa njia Mbadala wa kukabiliana na matatizo hayo.
Kamishna msaidizi wa kikosi cha usalama Bara barabi nchini Tanzania FORTUNATUS MUSLIM ambaye alikuwa mgeni Rasmi akizindua Rasmi na kutia Baraka kufanyika kwa Tamasha hilo |
Akizungumza wakati wa
uzinduzi wa Tamasha hilo Kamishna
msaidizi wa kikosi cha usalama Bara barabi nchini Tanzania FORTUNATUS MUSLIM ambaye
alikuwa mgeni Rasmi amepongeza Jitihada za kuanzishwa kwa mpango huo ambapo
amesema utawasaidia wao kama wahusika katika jitihada zao za kupambana na ajali
za barabarani nchini Tanzania.
Ameongeza kuwa Kikosi
cha usalama Barabarabi nchini Tanzania kimekuwa kikifanya Jitihada mbalimbali
za kupambana na ajali za Barabarani hasa kwa Bodaboda ambapo sasa wameanzisha
mashindano ya Mpira wa miguu maarufu kama Mpinga Cup ambayo yanalenga
kuwakutanisha madereva wa Bodaboda wote Jijini Dar es salaam ili kujifunza njia
za kuepukana na ajali ambapo amesema Tamasha la Pamoja Carnival limetia chachu
katika Jitihada hizo.
Tamasha la Pamoja
Carnival limedhaminiwa na FASTA FASTA ambao ni mfumo mpya wa usafiri Dar es salaam
ambao utawahakikishia wasafiri uhakika wa usalama wa safari zao,uhakika wa mali
zao,uhakika wa muda wao na madereva waaminifu.
Wadhamini wengine wa
Tamasha hilo ni PAMOJA APP ambayo ni njia ya kisasa ya kuwakutanisha watu na
wanaongea lugha ya Kiswahili nchini na Duniani kote pamoja na kutumia simu zao
za mikononi ambapo APP hiyo inasaidia kuwakutanisha watu waliopotezana na
kuongea na kubadilishana picha.
No comments:
Post a Comment