Na Vicent Macha wa HABARI24 BLOG
Serekali ya Tanzania
kupitia kwa wizara ya ujenzi uchukuzi na mawasiliano imeahidi kuendelea
kuisaidia mamlaka ya reli Tanzania na Zambia TAZARA katika kuboresha mamlaka
hiyo ikiwa ni pamoja na kufikia malengo na kuimarisha maeneo mbalimbali ikiwemo
kuwawezesha wafanyakazi wake nchini.
Hayo yamesemwa leo
Jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Msaidizi wa
Sehemu ya Usimamizi,
Ufuatiliaji na Tathimini wa Wizara ya ujenzi Uchukuzi, na
mawasiliano Bw.Aunyisa Meena,
wakati akifungua Rasmi maonyesho ya siku Tatu ya mamlaka Hiyo ikiwa ni sehemu
ya maadhimisho ya miaka 40 tangu kuanza kufanya kazi kwake ambapo amesema kuwa
serikali ya Tanzania pamoja na serikali ya Zambia zimejipanga kuhakikisha kuwa
zinamarisha mamlaka hiyo.
Meena
amesema kuwa katika kuhakikisha kuwa malengo ya kuboresha shirika hilo
yanatimia serikali ya Tanzania imeanza kupitia sheria ya TAZARA ili sasa
kuruhusu secta binafsi kuingia na kuwekeza ndani ya mamlaka hiyo ambapo amesema
kuwa kwa kuanza mpango huo Tayari serikali ya china imeanza kusaidia katika
sector hiyo huku serikali ikihitaji wadau mbalimbali watakaoweza kusaidia
mamlaka hiyo kusogeza mbele maendeleo yake.
Balozi wa China nchini Tanzania Dkt. Lu Youqing akihutubia katika shughuli hiyo CHINA ni moja kati ya nchi ambazo zimeonyesha nia ya dhati katika kuinua TAZARA kwa sasa |
Amesema
kuwa lengo la serikali ni kuhakikisha kuwa hali ya TAZARA inaimarika na kuwabadilisha
uelewa wafanyakazi wake ikiwa ni kipindi cha ushindani hivyo jitihada kubwa za
kuboresha ikiwemo kuwepo kwa mabehewa mazuri,njia nzuri,vichwa vizuri vya Treni
pamoja na mbinu mbalimbali ili kufanikiwa kuwapata wateja kutoka nchi za jirani
kutumia Treni za TAZARA katika kazi zake.
Bwana
Meena ameeleza kuwa mategemeo makubwa ya serikali ni kuhakikisha kuwa katika
kipindi kifupi TAZARA inaimarika huku akipongeza juhudi kubwa zinazofanywa na
TAZARA ikiwemo mpango wao wa sasa wa kurekebisha Engine zilizokuwa mbovu
zipatazo nne na sasa kuwezeshwa kufanya kazi.
Maonyesho
ya Miaka 40 ya TAZARA yalitanguliwa na shughuli mbalimbali miezi miwili
iliyopia zikiwemo uchagiaji wa damu,usafi katika Hospitali mbalimbali,ambapo
maonyesho ya leo yanalenga kuonyesha Shughuli na huduma mbalimbali zitolewazo na TAZARA.
Katika
uzinduzi huo leo umehudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo mabalozi akiwemo
Balozi wa Zambia nchini pamoja na Balozi wa China.
No comments:
Post a Comment