|
Regan Yudos Kutoka shule ya msingi Mbuyuni akipokea cheti na zawadi ya mshindi wa Pili katika shindano la kuandika Insha kwa shule za msingi aliyekabidhi zawadi hizo katika shughuli hiyo iliyofanyika katika Ofisi za Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano.leo tarehe 30 Agosti, 2016 ni Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu mawasiliano,Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi, na Mawasililiano Dr. Maria Sasabo Kushoto kwa mgeni rasmi ni Mwenyekiti wa Baraza Bw. Satanley Mwabulambo, kushoto kwa Mwabulambo ni Mjumbe wa Baraza Bw. Lawrence Mworia na kulia kwa mgeni rasmi Mary Shao Msuya Katibu Mtendaji wa Baraza hilo. |
|
Jane Michael Andrew mshindi wa kwanza katika shindano la kuandika Insha kwa shule za msingi akipokea cheti na zawadi kutoka kwa mgeni Rasmi Naibu Katibu Mkuu Mawasiliano Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi, na Mawasililiano Dr. Maria Sasabo leo Jijini Dar es salaam |
|
Felician Crispin Kapama kutoka Zanaki Secondary mshindi wa pili shindano la kuandika Insha kwa shule za secondary akikabidhiwa zawadi zake leo wakati wa utoaji wa zawadi hizo uliofanyika Ofisi za Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Jijini Dar es salaam |
|
Omary Abas Mdungu mshindi wa kwanza makala kwa vyuo vya elimu ya Juu akikabidhiwa zawadi zake Leo na mgeni Rasmi Naibu Katibu Mkuu Mawasiliano Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi, na Mawasililiano Dr. Maria Sasabo wakati wa Hafla hiyo fupi |
Baraza la Ushauri kwa Watumiaji
wa Huduma za Mawasiliano Tanzania ( TCRA CCC) leo limekabidhi vyeti na zawadi
kwa washindi walioshiriki katika shindano la uandishi wa insha kwa shule za
msingi na sekondari na makala kwa vyuo vya elimu ya juu katika mkoa wa Dar es
Salaam.
Mashindano hayo yalihusisha
washiriki kuandika insha na makala juu ya haki na wajibu wa watumiaji wa huduma
za mawasiliano hapa nchini.
Akikabidhi vyeti na zawadi hizo kwa washindi mgeni
rasmi, Naibu Katibu Mkuu Mawasiliano Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi, na
Mawasililiano DK. Maria Sasabo amesema amehamasika kuona vijana wameshiriki
katika mashindano hayo na kutoa maoni juu ya faida, changamoto na mbinu mbali
mbali za kukabiliana na changamoto hizo katika kuboresha utoaji wa huduma kwa
watumiaji wa huduma na bidhaa za mawasiliano.
Aidha, Dr. Sasabo ametoa rai kwa vijana kutumia fursa
mbali mbali zitokanazo na kukua kwa teknolojia ya habari na mawasiliano kukuza
vipaji, kujielimisha na pia kupata ajira.
Pia, amewaasa vijana kutumia huduma
mbali mbali za mawasiliano kwa kufuata sheria na kanuni za nchi kwa ustawi wa
wao kielimu, kijamii na kiuchumi.
No comments:
Post a Comment