Waandishi wa habari wakichukua matukio kwenye mkutano huo uliofanyika mapema leo jijini Dar es salaam. |
Katika kuhakikisha kuwa kila Mtanzania ambaye anapenda kushirki katika tamasha la Fiesta 2016 mdhamini mkuu wa tukio hilo la aina yake Tigo Tanzania leo imetangaza punguzo la asilimia kumi kwa tiketi itakayonunuliwa kwa Tigo Pesa kwa msimu huu wa Fiesta.
Tofauti na matukio yaliyotangulia, washiriki wote kutyoka mtandao wowote kwa tamasha la mwaka huu watakuwa na chaguo la kuzipata tiketi zao kupitia Tigo Pesa bila tozo za ziada.
Tiketi hizo zitawawezesha washiriki kulifikia kwa urahisi tamasha hilo ambalo litaanza rasmi Agosti 20, 2016 jijini Mwanza. Bei kamili za tiketi zitatangazwa hivi karibuni.
Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika Tip Top Manzese, Meneja Chapa wa Tigo William Mpinga alisema, “Njia ya kulipia tiketi kupitia Tigo Pesa lengo lake kubwa ni kuwapatia Watanzania njia rahisi na ya kawaida ya kupata tiketi zaoambayo ni ya kwanza na ya aina yake nchini Tanzania.”
Mpinga alibainisha kwamba huduma hiyo mpya imepanda chati kufuatia hivi karibuni kampuni hiyo ya simu kuanzisha kampeni ya NitigoPesa ambapo mtu yeyote kutoka mitandao mingine mikubwa nchini Tanzania anaweza kutuma na kupokea pesa kutoka kwa mteja wa TigoPesa.
Meneja chapa huyo aliongeza kwamba ikiwa kama kampuni ya mtindo wa maisha ya kidijitali Tigo inawahakikishia kuwa kwa kununua tiketi kupitia Tigo Pesa, wateja kutoka Tigo na mitandao mingine wataweza kuzifurahia huduma za Tigo Pesa bila tozo zozote za ziada.
Mpinga alieleza ili kununua tiketi kwa Tigo Pesa wateja kutoka mtandao wowote anatakiwa kupiga namba ya mfumo wa kifedha kwa njia ya simu (mfano: *150*01# kwa Tigo), chagua “Tuma Pesa” halafu chagua, “Mitandao mingine”, ikifuatiwa na, Tigo Pesa na hatua ya mwisho ingiza namba: 0678 888 888. Mbali na punguzo la asilimia kumi, wateja wa Tigo ambao watanunua tiketi za Fiesta kwa Tigo Pesa pia watapata kifurushi cha zawadi cha thamani ya shilingi 20,000 ambacho kinajumuisha dakika 400, SMS 400 na MB 400 zitakazotumika ndani ya siku saba.
Aliendelea kusema, “Kwa wateja wa mitandao mingine tiketi itakayonunuliwa kwa Tigo Pesa kutoka mitandao mingine watapata kadi ya 4G ikiwa na dakika 60 SMS 60 na MB 60 papo hapo pamoja na dakika nyingine 400, SMS 400 na MB 400 zitakazotumika ndani ya siku saba zikianza kutumika ndani ya saa 24”.
Huku akiwakaribisha Watanzania wote kushiriki katika Tamasha hilio la Fiesta, Mpinga aliwashauri washiriki kununua tiketi zao mapema ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza katika dakika za mwisho.
Tamasha la Tigo Fiesta 2016 linafanyika kwa ushirikiano kati ya Prime Time Promotions na Tigo Tanzania ambaye ni mdhamini mkuu.
No comments:
Post a Comment