Na Beatrice Lyimo – MAELEZO, Dodoma
Serikali imetoa wito kwa wanasiasa
kutotumia masuala ya Muungano katika masuala yao ya kiasisa kwani watu
wa pande mbili za Muungano hawawezi kufarakana kwa sababu ya umiliki wa
eneo.
Akijibu swali la Mhe. Jaku Hashim
Ayoub lililohusu umiliki wa kisiwa cha Latham (Fungu Mbarak), Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) January Makamba
amesema kuwa katika orodha ya changamoto 14 za Muungano
zilizoshughulikiwa na zinazoendelea kushughulikiwa hakuna suala lolote
linalohusu umiliki wa eneo.
Waziri Makamba amesema hakuna
mgogoro wowote unaohusu umiliki wa eneo lolote baina ya Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwa tafsiri
na suala zima la mipaka ya Jamhuriya Muungano wa Tanzania na Zanzibar
limewekwa wazi katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano na Katiba ya
Zanzibar.
Waziri Makamba amesema kuwa kuhusu
suala la mafuta na gesi hakuna mgogoro wowote kwani leseni za utafutaji
wa mafuta zilitolewa na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC)
katika eneo hilo kwa mujibu wa Sheria ya Utafutaji Mafuta na Gesi
Asilia ya mwaka 1980.
“Hakuna mgogoro wowote wa mafuta
na gesi baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali
ya Mapinduzi Zanzibar, huko nyuma leseni za utafutaji mafuta zilitolewa
na TPDC katika eneo hilo kwa mujibu wa Sheria ya utafutaji mafuta na
gesi asilia,” amefafanua Waziri Makamba.
No comments:
Post a Comment