Kimondo kilichopo Wilaya ya Mbozi Mkoani Mbeya.
……………………………………………………………..
Na Beatrice Lyimo-MAELEZO, Dodoma.
Serikali inaendelea kutangaza
Kimondo kilichopo Wilaya ya Mbozi Mkoani Mbeya ikiwa ni kivutio muhimu
na adimu nchini na duniani kwa ujumla.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa
Maliasili na Utalii Mhandisi Ramo Kamani leo mjini Dodoma alipokuwa
akijibu swali la Mbunge wa Vwawa Mhe. Japhet Hasungu lililohusu mpango
wa Serikali katika kuhamasisha watalii wa ndani na nje kuja kuangalia
Kimondo hicho.
Naibu Waziri huyo amesema kuwa
Serikali imekuwa inaendelea kuhamasisha kwa kukitangaza Kimondo hicho
kwa kutumia njia mbalimbali ikiwemo vipindi vya runinga na nakala za
machapisho mbalimbali.
“Uhamasishaji umefanyika kwa
kutumia njia mbalimbali ndani na nje ya nchi ikiwa ni pamoja na vipindi
vya runinga vya ZAMADAMU na Utalii wa ndani na kutumia machapisho ya
Tanzania ya “The land of great Heritage Sites” na “Tanzania Cultural
Heritage Resources” ambapo nakala zake husambazwa katika maonesho
mbalimbali na Balozi zetu pamoja na jarida la “Ifahamu Idara ya mambo ya
kale”” na jarida la Maliasili,” alifafanua Naibu Waziri huyo.
Aidha, Mhandisi Kamani aliongeza
kuwa juhudi hizo limepelekea ongezeko la idadi ya watalii na mapato
ambapo kati ya mwaka 2012/2013 na 2014/2015 watalii waliongezeka kutoka
990 hadi 1,681 pamoja na mapato kuongezeka kutoka shilingi 811,000 hadi
2,426,00.
Mbali na hayo, Mhandisi Kamani
alitoa wito kwa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi na wadau wengine
kujitokeza kuboresha mazingira na miundombinu ya eneo la kimondo hicho
ili kuweza kuzidi kuvutia watalii wengi na kuongeza pato la taifa.
Kimondo hicho kinaendelea kuiweka
Tanzania katika ramani ya dunia katika masuala ya utalii ambapo
kinaaminiwa kuwa ni kati ya vimondo nane vikubwa zaidi duniani
kinachokadiriwa kuwa na uzito wa tani 12, urefu wa mita 3.3, upana wa
mita 1.63 na kimo cha mita 1.22
No comments:
Post a Comment