Licha ya kucheza kwenye uwanja wa nyumbani, Mbao Fc ya Mwanza imejikuta ikishindwa kuhimili vishindo vya Mbeya City Fc na kukubali kufungwa mabao 4-1 kwenye mchezo wa ligi kuu ya soka Tanzania bara uliochezwa leo hii kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini hapa.
Kwenye Mchezo huo ulioanza kwa kasi timu zote zikishambuliana kwa zamu, wenyeji walikuwa wa kwanza kulifikia lango la City baada ya Vicent Philipo kufanikiwa kumtoka Haruna Shamte aliyekuwa anacheza beki ya kulia lakini mpira wa krosi wa mchezaji huyo wa Mbao uliishia mikononi mwa kipa Owen Chaima.
City ilijibu shambulizi kwenye dakika ya 20 kupitia Ayoub Semtawa aliyefanikiwa kuwatoka walinzi wa Mbao Fc lakini mpira aliompenyezea Omary Ramadhani uliokolewa na walinzi wa timu hiyo mwenyeji kabla ya Raphael Daud kufanikiwa kuandika bao la kwanza baada ya kuunganisha mpira ulikuwa umepigwa na Ayoub Semtawa kwenye dakika ya 28, bao lililodumu kwa dakika 10 baada ya Vicent Philipo kuswazisha dakika ya 38 na kumaliza kipindi cha kwanza timu zote zikiwa na bao 1-1.
Kipindi cha pili Kocha Kinnah Phiri alifanya mabadiliko ya kumtoa alifanya mabadiliko ya kumtoa Ayoub Semtawa na nafasi yake kuchukuliwa na Ditram Nchimbi mabadiliko ambayo yaliongeza uhai kweny safu ya ushambuliaji kwani dakika chache baadae Omary Ramadhani aliiandika bao la pili, bao lilofuataiwa na mabao mengine mawili kutoka kwa Ramadhani Chombo na Raphael Daud waliohitimisha dakika 90 ubao ukisomeka mabao 4 kwa City na 1 kwa Mbao Fc.
Mara baada ya mchezo huo kocha wa City Kinnah Phiri, pamoja na mengine mengi lakini pia aliwapongeza wachezaji wake kwa kucheza vizui kwa kufuata Maelekezo na hatimaye kuibuka na ushindi huo mnono.
“Vijana wangu wamecheza vizuri, wamefanya kazi kwenye kila tulichokuwa tunakifanyia mazoezi, tulijua Mbao wangekuja na mchezo wa kasi kwa sababu walihitaji sana kushinda hasa baada ya kupoteza mchezo wao uliopita, tunamshukuru Mungu kwa kutuwezesha kupata pointi saba kwenye michezo yetu mitatu na sasa tunarudi nyumbani kujiandaa na mchzo mwingine”, alisema.
Dondoo za mchezo,mahojiano ya Kinnah Phiri yapo hapa : http://mbeyacityfc.com/event/mbao-fc-vs-mbeya-city/
City itaondoka Mwanza alfajiri ya kesho kuelekea jijini Mbeya tayari kwa matayarisho ya mchezo dhidi ya Azam Fc uliopangwa kuchezwa tarehe 10 mwezi huu kwenye uwanja wa Sokoine.
No comments:
Post a Comment