Kwenye mchezo huo uliokuwa na kasi ya aina yake, timu zote zilianza dakika 45 za kwanza kwa nguvu kubwa iliyoacha mashambilizi ya kila mara pande zote mbili lakini uimara wa walinda milango, Owen Chaima na Shaban Kado ulifanya washambuliaji wa timu zote kushindwa kufunga mabao ya mapema.
Dakika ya 27, mpira ulioanzia upande wa kulia kwa John Kabanda aliyefanikiwa kuupitisha vizuri katikati ya uwanja kwa nahodha Kenny Ally, ulifanikiwa kufika kwenye miguu ya Ditram Nchimbi ambaye akiwa nje kidogo ya eneo la 18 la Mwadui Fc alifumua shuti kali lililomshinda kipa Kado na kutinga wavuni moja kwa moja,kuandika bao la kwanza kwa City lililodumu hadi mwisho wa kipindi cha kwanza.
Kipindi cha pili, kocha wa City Kinnah Phiri alifanya mabadiliko kwa kumtoa, Joseph Mahundi na nafasi yake kuchukuliwa na Hamidu Mohamed pia alimtoa Omary Ramadhani na kuingia Salvatory Nkulula huku Rajab Zahir aliyepata majeraha akimpisha Ramadhani Chombo, mabadilliko yaliisaidia timu yake kuimarisha safu ya kiungo na hatimaye kufanikiwa kukamilisha dakika 90 matokeo yakibaki kama yalivyokuwa.
Mara baada ya mchezo kocha msaidizi Mohamed Kijuso, alisema wachezaji wake wamecheza vizuri kwa kufuata maelekezo jambo lililochangia kupatikana kwa ushindi huu.
“Mchezo ulikuwa mzuri, vijana wamecheza kwa kufuata maelekezo ya Mwalimu, hili limetusaidia kuibuka na ushindi,hatukuwa vizuri kipindi cha pili lakini safu yetu ya ulinzi ilisimama imara kufuta makosa yote, huu ni wakatri mwingine wa kuijiandaa na mchezo ujao kwa sababu tayari tuna nguvu na ari kubwa kufuatia ushindi wa leo “alisema.
Katika hatua nyingine kocha wa Mwadui Fc , Jamhuri Kihwelo alitangaza kujiuzuru kuifundisha timu hiyo huku akiapa kutokujihusisha tena naa mchezo wa soka nchini kwa kile alichookita kuchoshwa na upindishaji wa sheria 17 za soka aliyodai unafanywa kwa makusudi na waaamuzi wa soka licha ya kukiri kutokuwa na tatizo lolote na bao alifungwa kwenye mchezo wa jana.
Kocha Julio alisema kuwa ameaamua kuachana na soka la nchi hii kwa sababu haoni dalili za kusonga mbele kutokana na matatizo ya watu wacheche huku akijisifu kwa kupata mafanikio makubwa kwenye kazi yake hiyo aliyoifanya pia kwenye mataifa mbalimbali ikiwemo Qatar, Yemen na nchi kadhaa za Falme za kirabu.
Kocha Julio alisema kuwa ameaamua kuachana na soka la nchi hii kwa sababu haoni dalili za kusonga mbele kutokana na matatizo ya watu wacheche huku akijisifu kwa kupata mafanikio makubwa kwenye kazi yake hiyo aliyoifanya pia kwenye mataifa mbalimbali ikiwemo Qatar, Yemen na nchi kadhaa za Falme za kirabu.
No comments:
Post a Comment